Serikali ya Kenya imethibitisha kujiandaa kikamilifu kufanikisha malipo ya ada ya kuhudumia Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2027, huku ikikabiliwa na tarehe ya mwisho ya 30 Machi 2026. Kenya inatakiwa kulipa Ksh3.9 bilioni (takriban $30 milioni) kabla ya tarehe hiyo, huku washirika wake, Tanzania na Uganda, tayari wamelipa ada zao.
Kupitia katibu mkuu wa wizara ya michezo Elijah Mwangi amesema kwamba wamepatiwa muda hadi kufikia tarehe 30 machi wawe wameshalipa hela hiyo ya kuhudumia michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tumepatiwa hadi tarehe 30 Machi kulipa ada ya kuhudumia AFCON. Tunaelewa kuwa nchi zetu ‘Pamoja’, Uganda na Tanzania, tayari wamelipa, lakini Kenya bado haijalipa sehemu yake ya Ksh3.9 bilioni. Hivyo, mafanikio tuliyoyapata hadi sasa katika maandalizi ya AFCON yanaweza kuhatarishwa ikiwa hatutaweza kulipa kabla ya tarehe hiyo, na mawasiliano tuliyo nayo kutoka CAF yanaonyesha lazima tuchukue hatua.”
Mwangi pia alifafanua kuwa tatizo haliko kwenye upungufu wa fedha, bali fedha hizo haziko kwenye bajeti ya sasa ya serikali. “Hili si tatizo kubwa kwani serikali ina fedha, changamoto ni kwamba haziko kwenye bajeti yetu ya sasa,” alisema. Aliendelea kueleza kuwa katika kipindi hiki cha bajeti ya ziada, fedha hizo zitapewa kipaumbele.
Aidha, Mwangi alisisitiza kuwa Kenya, pamoja na Uganda na Tanzania, waliwasilisha maombi ya kushiriki kama nchi zinazoshirikiana (Pamoja) kuhost AFCON 2027. Wenyeji wengine tayari wamelipa ada zao, na Kenya ina muda hadi 30 Machi kulipa kiasi kinachohitajika.
Katibu Mwangi aliweka bayana kuwa hakuna haja ya wananchi wa Kenya kuwa na hofu “Hakuna sababu ya kuwasumbua. Kuna muda wa kutosha kupata fedha na kulipa kabla ya tarehe 30 Machi. Wakenya wasiwe na wasiwasi.”
Mashindano haya ya AFCON, ambayo yatafanyika kati ya 19 Juni hadi 18 Julai 2027, yatakuwa ya kwanza kuandaliwa na nchi tatu, na ya kwanza baada ya miaka hamsini kuandaliwa katika ukanda wa CECAFA tangu Ethiopia kuhost mwaka 1976. Tukio hili pia litakuwa sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Kombe la Mataifa Afrika, na ni AFCON ya mwisho kufanyika katika mwaka usio wa jozi, kwani kuanzia 2028 mashindano yatafanyika kila miaka minne.

