McCarthy: Lengo la Kenya Si Kushinda Kila Mchezo, Bali Kujenga Kikosi Imara

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Benni McCarthy, ameeleza umuhimu wa michuano ya FIFA Series huku timu yake ya Kenya ikijiandaa kuvaana na timu ya taifa ya Estonia katika mchezo utakaopigwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali nchini Rwanda. Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya kimataifa ijayo.

McCarthy: Lengo la Kenya Si Kushinda Kila Mchezo, Bali Kujenga Kikosi ImaraMcCarthy amesema kuwa mashindano hayo ni fursa muhimu kwa mataifa ya Afrika kujipima dhidi ya timu kutoka mabara mengine, hususan Ulaya na Caribbean. “Huu ni mpango mzuri sana kutoka FIFA kwa sababu unatoa nafasi kwa nchi za Afrika kucheza dhidi ya timu kutoka mashirikisho mengine, ikiwemo Ulaya na Caribbean,” alisema McCarthy.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Ameongeza kuwa mechi dhidi ya Estonia itakuwa kipimo sahihi kwa timu yake, akibainisha kuwa wapinzani wao wamekuwa wakicheza dhidi ya mataifa makubwa ya Ulaya. “Unapocheza dhidi ya timu za Ulaya, kama Estonia ambao walikutana na Cyprus, Norway na Italy, ni kipimo kizuri kujua tupo wapi kama taifa,” alisisitiza.

McCarthy: Lengo la Kenya Si Kushinda Kila Mchezo, Bali Kujenga Kikosi ImaraKocha huyo wa zamani wa wasaidizi wa Manchester United alieleza kuwa wachezaji wake wanapaswa kuitumia fursa hiyo kujifunza na kuboresha kiwango chao. “Ni nafasi ya kipekee kwetu kujipima dhidi ya timu bora ya Ulaya, itakuwa changamoto kubwa lakini pia somo muhimu kwa wachezaji wetu,” alisema.

Aidha, McCarthy amebainisha kuwa lengo kuu kwa sasa si kushinda kila mchezo bali ni kujenga timu imara kuelekea AFCON 2027 ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania. “Kwa sasa ni kuhusu kuwa tayari kushindana, kujifunza na kuendelea kuboresha kikosi chetu,” aliongeza.

McCarthy: Lengo la Kenya Si Kushinda Kila Mchezo, Bali Kujenga Kikosi ImaraAkihitimisha, McCarthy amesema kuwa uzoefu unaopatikana katika mashindano kama FIFA Series utakuwa muhimu sana kwa maendeleo ya timu hiyo. “Tunataka ifikapo 2027 tuwe katika nafasi ya kusema tunalenga kushinda mechi nyingi za hatua ya makundi, lakini kwa sasa tunajifunza na kujijenga,” alimalizia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.