Mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Lamine Yamal, amelaani vikali tabia ya baadhi ya mashabiki waliokuwa wakiimba nyimbo zenye dhihaka dhidi ya Waislamu wakati wa mchezo wa jana.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Yamal alisema “Mimi ni Muislamu, Alhamdulillah. Jana uwanjani kulisikika wimbo ‘asiyepiga kelele ni Muislamu’. Najua ulikuwa unalenga wapinzani, lakini kwangu kama Muislamu bado ni ukosefu wa heshima na jambo lisilokubalika.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Nyota huyo kijana aliongeza kuwa ingawa si mashabiki wote wanaoshiriki vitendo hivyo, bado kuna haja ya kubadili mtazamo. “Ninaelewa si mashabiki wote wako hivyo, lakini kwa wanaoimba mambo kama haya, kutumia dini kama mzaha kunawafanya muonekane wajinga na wabaguzi,” alisisitiza.
Yamal alieleza kuwa mpira wa miguu unapaswa kuwa jukwaa la kuunganisha watu wa tamaduni na dini mbalimbali badala ya kuwa chanzo cha migawanyiko. Kauli yake imeibua mjadala mpana kuhusu maadili ya mashabiki viwanjani.
Aidha, alitoa pongezi kwa mashabiki waliokuja kutoa sapoti kwa njia ya heshima na kuonesha mapenzi ya kweli kwa timu yao bila kuvuka mipaka ya utu na maadili.
Akihitimisha, Yamal alisema “Mpira ni burudani na unatakiwa kuleta watu pamoja, si kuwagawa. Nawashukuru mashabiki waliotuunga mkono na tutakutana tena kwenye mashindano yajayo ya Kombe la Dunia.”

