Kocha wa Feyenoord, Robin van Persie, ameweka wazi kuwa anatarajia makubwa zaidi kutoka kwa winga Raheem Sterling, ambaye bado hajafikia kiwango kilichotarajiwa tangu ajiunge na klabu hiyo. Nyota huyo wa England ameendelea kuwa gumzo kufuatia kiwango chake kisichoridhisha katika mechi za hivi karibuni.

Licha ya kiwango kibovu, Van Persie hajamkatia tamaa mchezaji huyo mwenye uzoefu mkubwa. Ameeleza kuwa anafanya kazi kwa karibu sana na Sterling ili kuhakikisha anarudi kwenye ubora wake, akisisitiza kuwa mchezaji huyo anaelewa wazi nini kinahitajika kuboreshwa.
Baada ya mchezo wa De Klassieker dhidi ya Ajax uliomalizika 1-1, Van Persie alifanya mazungumzo ya kina na Sterling, akimweleza moja kwa moja matarajio yake. Kocha huyo amesema anampa maelekezo ya wazi na makali, akiamini kuwa wachezaji wakubwa wanapaswa kuhimili presha hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hadi sasa, Sterling amecheza dakika 256 tu katika mechi tano rasmi, huku mchango wake mkubwa ukiwa asisti moja muhimu dhidi ya Excelsior. Hii inaonyesha bado hajapata muendelezo wa kiwango unaohitajika kuisaidia timu.

Kwa mechi sita zilizobaki msimu huu, presha iko juu kwa Sterling kujidhihirisha na kusaidia Feyenoord kufikia lengo lao la kufuzu Ligi ya Mabingwa. Huu ndio wakati wake wa kuthibitisha kuwa bado ana uwezo wa kuwa mchezaji wa kiwango cha juu.

