Uongozi wa Real Betis umeanza harakati za haraka kuhakikisha wanamnunua moja kwa moja kiungo wa Morocco, Sofyan Amrabat, kabla ya mkopo wake kutoka Fenerbahçe kumalizika mwezi Juni. Nyota huyo ameonekana kuwa mhimili muhimu ndani ya kikosi.

Kwa mujibu wa ripoti, Betis wamempa kipaumbele cha juu Amrabat katika mipango yao ya usajili wa majira ya joto, wakivutiwa na mchango wake mkubwa uwanjani pamoja na ushawishi wake ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo. Ameonekana kama kiongozi halisi wa timu licha ya kuwa kwa mkopo.
Sababu nyingine inayochochea uharaka wa mazungumzo hayo ni Kombe la Dunia 2026. Betis wana hofu kuwa kama Amrabat ataonyesha kiwango kikubwa akiwa na Morocco, thamani yake itapanda sana na kufanya dili kuwa gumu zaidi baadaye.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa zinaeleza kuwa klabu tayari imewasiliana na mchezaji pamoja na wakala wake, na imepata mwanga wa awali kuendelea na mazungumzo rasmi na Fenerbahçe. Hii inaonyesha uwezekano mkubwa wa makubaliano kufikiwa ndani ya muda mfupi.

Iwapo kila kitu kitaenda sawa kifedha, Betis wanaweza kutangaza rasmi usajili huo siku chache zijazo, hatua itakayowahakikishia kubaki na mmoja wa wachezaji wao muhimu kabla ya soko la usajili kuchangamka zaidi.

