Spurs Wapoteza Tena, De Zerbi Ataja Suluhisho

Kocha mpya wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji msaada wa karibu zaidi wa kisaikolojia kama wa “baba” badala ya maelekezo ya kawaida ya ukocha, kufuatia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Sunderland AFC.

Spurs Wapoteza Tena, De Zerbi Ataja SuluhishoDe Zerbi alichukua mikoba ya ukocha mwishoni mwa mwezi uliopita akichukua nafasi ya kocha wa muda Igor Tudor, lakini alianza vibaya baada ya Spurs kupoteza mchezo huo uliowaacha katika hatari ya kushuka daraja kwenye Premier League.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bao pekee la mchezo lilifungwa kipindi cha pili na Nordi Mukiele, likiwa limepata mguso uliobadili mwelekeo, na kuifanya Tottenham kubaki nyuma kwa pointi mbili dhidi ya West Ham United huku zikiwa zimesalia mechi sita pekee msimu huu.

Spurs Wapoteza Tena, De Zerbi Ataja SuluhishoSpurs hawajapata ushindi wowote wa ligi tangu Desemba mwaka jana, na sasa wanakabiliwa na hatari ya kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1977, jambo linaloonyesha ukubwa wa changamoto aliyonayo De Zerbi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, De Zerbi alisisitiza kuwa ushindi mmoja unaweza kubadilisha hali ya timu hiyo.
“Tunapaswa kupigania ushindi mmoja kwa sababu ushindi mmoja unaweza kubadilisha kila kitu msimu huu,” alisema.

Spurs Wapoteza Tena, De Zerbi Ataja SuluhishoKocha huyo alikiri kuwa timu yake ina ubora lakini inakosa kujiamini, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na kujiamini zaidi.
“Wachezaji wana ubora mkubwa, lakini tunapaswa kujiamini zaidi. Jambo muhimu zaidi sasa ni kushinda mechi moja,” aliongeza.

Spurs Wapoteza Tena, De Zerbi Ataja SuluhishoDe Zerbi pia alieleza kuwa changamoto kubwa si uwezo wa soka bali ni hali ya kisaikolojia ya wachezaji wake.
“Naweza kuwa kama kaka au baba kwao, hawahitaji kocha kwa sasa. Hawahitaji kuboresha soka lao, watafanya vizuri zaidi tutakapopata kujiamini,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.