Barcelona Watoa Dozi Nyingine!

 

Ni mwendo wa dozi! Frankie De Jong ambaye amejiunga na Barcelona kuanzia msimu ujao ameendeleza historia mbovu kwa Madrid kwa kuiondoa kabisa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Barcelona kupitia usajili wao waliweza kufanya maangamizi hayo yaliyowaacha vichwa chini Madrid wakiwa hawana nafasi ya kushinda kikombe kwa sasa ndani ya msimu huu.

Kwa mara kwanza ndani ya siku 1393 Madrid ndio wametolewa ndani ya mashindano makubwa hayo huku wakiwa wameshinda mara tatu mfululizo kombe hilo ndani ya siku za hivi usoni. Wakiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo tangu ilipomtokea Bayern Munich miaka ya 1970.

Madrid walionekana kama wangeweza kufanya vizuri zaidi kutokana na kutokuwa na nafasi tena kwenye baadhi ya vikombe vingine katika msimu huu lakini mambo yanaonekana kwenda ndivyo sivyo kwao kwa awamu nyingine. Hakuna aliyefikiri kwamba Madrid angeweza kutolewa katika hatua hiyo na mapema kiasi hicho.

Frankie De Jong akikiongoza kikosi chao alifanya kazi kubwa sana ya kuwaondoa kabisa mchezoni viungo wa Madrid na kuonekana wakiwa wameutawala mchezo kitu ambacho kinamfanya mchezaji huyo ambaye amesaini tayari kuichezea Barcelona kuonekana kama tayari yupo upande huo wa Catalunya na akiwa anawapa salamu za awali pindi atakapojiunga na upande huo.

Muunganiko wa kikosi chao ulikuwa ni wenye kuvutia ambapo Dusan Tadic akiwa katika nafasi yake aliiwezesha timu yake kwa kutengeneza magoli mawili yaliyowapeleka mbele zaidi huku safu ya ulinzi iliyoongozwa na Matthijs de Ligt iliwamuDu kabisa washambuliaji wa Madrid wasipenye kwenye lango lao.

Miaka ya 1960 Madrid walishinda kombe la Ulaya lakini wakiwa katika harakati la kutafuta kikombe cha sita ndani ya msimu huo walipoteza mechi yao mbele ya Barcelona ambao walikuwa wanakitafuta sana kikombe hicho. Lakini, pia kwa awamu nyingine wameweza kupoteza mechi yao nyingine wakiwa katika hatua muhimu mbele ya timu yenye jina lilelile.

Barcelona walipunguzwa kasi yao ya ushindi waliyokuwa nayo miaka 59 iliyopita lakini inaonekana utawala wake huo umerejea tena miaka hii ya 2019 kutokana na matokeo anayoyapata akiwa ugenini na nyumbani pia, ambapo wiki lililopita aliwaondosha kwenye Copa del Rey na akaweza kufukia ndoto zake za kutetea ubingwa. Kwa mara nyingine tena mchezaji wao anahusika kumuondoa kwenye mashindano ya klabu bingwa hasimu wake.

Modric alipotezwa kabisa na kiungo huyo pamoja na ubora aliokuwanao kwa siku za hivi usoni. Lakini wenzake, Kroos na Casemiro walifichwa kabisa na kufanya kazi yao kuwa ngumu sana katika eneo la kiungo kitu ambacho ni nadra sana kwa Madrid kukutana nacho uwanjani.

 

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.