Nusu Fainali ya FA

Ikiwa klabu nyingine zimetupwa tayari katika michuano hiyo inayoelekea mwishoni nchini Uingereza, makundi ya hatua ya nusu fainali tayari yameanikwa na kila mmoja amejua wa kukutana naye katika hatua hiyo muhimu. Kwa sasa kila mmoja amejua mbaya wake ambaye aidha atamtupa nje ya michuano au atatupwa nje ya kombe hilo lililofikia hatua nzuri na nyeti sana.

Ndani ya mechi hizo imeonesha wazi United wakishindwa kuwika mbele ya wageni wao Wolves ambao walicheza mechi yao wakiwa na nia moja tu ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo; na Watford wakifanikiwa kuandika historia yao ya kufuzu katika michuano hiyo na kuwafanya wasonge mbele ikiwa ni historia yao kubwa sana kwa kipindi hiki ndani ya michuano hiyo.

Katika hatua hiyo makundi yamepangwa tayari baada ya mechi kuchezwa na kufikia hadi hatua ya mikwaju ya penati jambo ambalo linaonesha ugumu wa michuano hiyo kwa sasa na utayari wa kila klabu kutaka kupata matokeo ndani ya mechi pale inapobidi kutokea. Wamekuwa mwiba kwa klabu nyingi ndani ya msimu huu hakika.

Kwa hatua hiyo sasa, Manchester City watacheza dhidi ya Brighton & Hove Albion kuelekea hatua ya fainali ambapo ni dhahiri kwamba hii inaonekana kuwa mechi rahisi sana kwa City ambaye kiwango chake na aina ya kikosi alichonacho bado vinampa nafasi kubwa sana kuweza kufanya vizuri sana kwenye michuano hiyo.

Kundi jingine ni kati ya Wolverhampton Wanderers watakutana na Watford; wababe hao wa United kama wakitumia nafasi na kucheza soka kama walilocheza mbele ya United kwa nguvu ile ile wataweza kusonga mbele na kupenya hadi hatua ya nusu fainali maana wanayekutana naye uwezo wake wanaendana kwa hiyo ni mpinzani wa kiwango chake kabisa.

City amepenya kwa kile kinachofahamika kama mapinduzi ya kisoka baada ya kuchezeshewa kipigo cha 2-0 katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kitu ambacho sio cha kawaida kwao; lakini waliweza kurejea mchezoni na kupata ushindi mbele ya mpinzani wake na kuwasaidia kusonga mbele katika michuano hiyo.

Lakini upande wa matajiri wenzake walishindwa kabisa kupenya mbele ya himaya ya Wolves na kuwafanya kuendelea na rekodi mbovu ya kupoteza mechi zake ambapo alianza na ile ya Arsenal na hadi hiyo ya michuano ya FA kitu ambacho kimeanza kuchafua rekodi ya kocha huyo mpya anayeonekana kufanya vizuri. Kama hali itaendelea hivyo United kwa msimu huu hawana nafasi ya kumaliza msimu wakiwa na kikombe chochote.

Mechi zote mbili zinategemewa kuchezwa Aprili, 6 na 7 na kila mshindi kwenye mechi hizo atapata nafasi ya kukutana na mwenzake kwenye fainali itakayochezwa Mei, 18. Katika hatua hiyo, City anaonekana kupigiwa sana upatu wa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo na kwa hali ilivyo anaweza kunyanyua kikombe hicho.

2 Komentara

    Mambo ni moto

    Jibu

    Lazima kiwake maana sio powa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.