Ilikuwa ni siku mbaya upande wa Sarri ambaye alipata kipigo mbele ya Everton waliokuwa kwenye ubora wa hali ya juu ambao haujawahi kushuhudiwa kwao wakiwa nyumbani hususan wanapocheza na klabu kubwa. Huu ni ushindi wao wa kwanza tangu Januari wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Chelsea walitawala mechi hiyo kwa kipindi kizima cha kwanza huku Hazard akipata nafasi iliyoshuhudia mpira ukiishia kugonga mlingoti wa magoli yaliyokuwa chini ya mlinzi mwenye historia kubwa katika taifa la Uingereza, Pickford wakati pia akiokoa mipira mingi kutoka kwa Higuain.
Pedro alijitahidi kufurukuta angalau awape ushindi Chelsea lakini juhudi zake hazikuzaa matunda kabisa mbele ya Everton walioonekana kuwa na kiu kubwa ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo. Pedro goli lake lilikataliwa na mwamuzi kwamba mchezaji huyo aliotea mpira ule na ikaamuriwa urudishwe kuashiria sio goli.

Dakika nne pekee za kipindi cha pili zilitosha kuwapa uongozi Everton kupitia kwa mchezaji wao Richarlison ambaye aliunganisha mpira pekee uliokuwa umechezwa kwa kichwa na Dominic Calvert Lewin ambao baadaye uliweza kuchezwa na Kepa lakini haukufanikiwa kwenda mbali na kujikuta unaangukia kwenye himaya ya wapinzani waliofanikiwa kuweka nyavuni goli lao la kwanza.
Iliwachukua muda kupata goli jingine ambapo dakika ya 70 ya mchezo walifanikiwa kuandika goli jingine baada ya kuzawadiwa mpira wa adhabu baada ya Marcos Alonso kumchezea ndivyo sivyo katika eneo la hatari Richarlison ambaye alikuwa mwiba sana kwenye mechi hiyo huku akiisumbua sana safu ya ulinzi ya klabu hiyo.
Pamoja na kuanza vibaya katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo lakini walifanikiwa kurudi kimchezo kwenye umiliki wa mchezo na kuwafanya kufunga magoli hayo mawili ndani ya mchezo huo ambao ulimwacha mdomo wazi Sarri ambaye msimu huu amekuwa na kibarua kizito kinachohatarisha hata kibarua chake.
Walionesha umakini na uthubutu katika mechi hiyo baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha msimu huu hasa ikikumbukwa wametoka kupokea kichapo katika mchezo wao uliopita dhidi ya Newcastle United ambao walimpa kichapo cha 3-2 lakini hilo halikuwazuia wao kurudi mchezoni haraka dhidi ya klabu hiyo kubwa.
Kipigo hicho ni dalili mbaya kwa Chelsea kwani matumaini yake ya kusalia nafasi nne za juu kwenye ligi hiyo kwani hadi sasa idadi ya mechi imalingana na wengine lakini wanatofautiana alama ambapo Arsenal yupo juu yao akiwa na alama zake 60, United wanafuata wakiwa na alama 58 na wao Chelsea wana alama zao 57; huku akiwapisha wawili hao kuendelea kupambania nafasi za juu. Kazi ipo pale juu!


Povel
Ngoj tuone
Furahav
Noma