Raha za FA Cup…

Michezo ya kombe la FA ilishika kasi huku ikishuhudiwa baadhi ya klabu kubwa zikipata shida mbele ya klabu ambazo zinachukuliwa kuwa na uwezo wa chini. Klabu zenye majina makubwa zimepata shida kupata matokeo mbele ya klabu ambazo mara nyingi hupata shida kuchukua alama mbele ya klabu hizo.

Katika hatua hiyo ya mtoano, Watford waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuwapa dozi Crystal Palace ya 2-1 kitu ambacho kiliwatupa nje ya michuano hiyo. Mechi ya wawili hao ilitawaliwa na ufundi mkubwa huku klabu hizo zikishambuliana kwa zamu na kasi kubwa sana lakini hadi kipyenga cha mwisho Watford walifanikiwa kuondoka na ushindi.

Mechi nyingine iliyokuwa ya kuvutia ni kati ya Swansea City waliokuwa wenyeji wa Manchester City. Katika mechi hiyo Swansea walionesha ukomavu wao mkubwa sana katika soka baada ya kuwasumbua sana Man City hadi kufanya mechi kuwa na idadi kubwa ya magoli. Jambo hilo lilionekana kuwashangaza mashabiki wengi wa soka.

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha City alikuwa amelala kwa goli 2-0, jambo ambalo sio la kawaida kwa timu kubwa na yenye kikosi kipana kama Man City. Lakini, haikuishia hapo kipindi cha pili walijaribu kusawazisha makosa yao na kufanikiwa kurudisha magoli yao yote waliyofungwa kipindi cha kwanza.

FA

Huku mechi yao ikiwa inaelekea kuisha na matokeo yakiwa 2-2, wakati wa dakika za mwishoni kabisa mwokozi wa mara nyingi wa timu hiyo Sergio Aguero alipachika goli lake dakika ya 88 ya mchezo na kuokoa jahazi hilo hivyo kuwafanya City kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa 3-2.

Mechi nyingine iliyokuwa ngumu na yenye kustaajabisha ni ile kati ya ya Wolves na Manchester United ambapo iliwafanya United kushindwa kabisa kutamba nyumbani na kutolewa kwenye michuano hiyo mikubwa sana Uingereza. Wolves walionesha kandanda safi sana ambalo liliwafanya United kushindwa kabisa kupenya.

Walikuwa ni  Raul Jimenez na Diogo Jota waliotumia kipindi cha pili vizuri kuipa timu yao ushindi mbele ya United walioonekana kumiliki sana mpira lakini wakakosa uimara katika eneo la ushambuliaji na kuwafanya wageni wa mchezo huo kuondoka na ushindi wa 2-1 kutokana na kuwa na mipango iliyoonekana wazi kabisa kwamba walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote.

Klabu ambazo hadi sasa zimefanikwa kupata matokeo na kusonga mbele ni Watford, Manchester City na Wolves huku wakisubiri mechi nyingine ili kujua hatma ya safari yao kwenye michuano hiyo. Kwa hali ilivyo, City anaweza akawa hana mpinzani kwa hatua hiyo na kuna uwezekano akanyanyua kombe hilo.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.