Kitu nadra sana hiki, klabu yako inafungwa na unashangilia goli ambalo umefungwa na mpinzani wako! Huyu ndiyo Messi akikamilisha hattrick yake, wakati mwingine mafundi wanapaswa kupokea pongezi zo tu bila hiyana.
Hii imetokea kwenye gemu ya Jumamosi kati ya Real Betis na Barcelona pale ambapo mashabiki wa Real Betis waliposhindwa kujizuia kumshangilia mtambo wa Barcelona, Lionel Messi alipokamilisha goli lake la tatu kwenye gemu hiyo -Hattrric kwenye ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Real Betis.

Uwanja mzima ulifunikwa na sauti za “Messi! Messi! Messi!….” pale Benito Villamarin ndani ya mji wa Seville baada ya messi kucheka na nyavu kwa mara ya tatu dakika ya 85 na kukamilisha jumla ya hattrick 33 kwenye LaLiga huku akifikisha jumla ya hattrick 45 kwa Barcelona na hattric ya 51 kwa maisha yake ya soka la kulipwa.
Kwa hisia Messi alinukuliwa akisema kuwa hilo ni jambo geni kabisa kwake baada ya kuulizwa kuhusu kilichotokea kwa mashabiki wa Betis.
“hapana, sikumbuki kama hii imewahi kiujitokeza hapo nyuma. Najihisi fahari, huwa wanatupokea vizuri wakati wote tukiwa tunacheza hapa”
Ushindi dhidi ya Real Betis umeendelea kuwaweka Barca kileleni kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya Atletico Madrid ambao wako nafasi ya 2 wakati wakiwa na gemu 10 zilizobaki.


Devotha
Laliga ni moto