Zikiwa zimesalia mechi chache kuelekea kuhitimisha mzunguko wa msimu wa 2018/19 bado kuna wakati mgumu kujua nani ataibuka mshindi wa kombe hilo ambalo msimu huu linaonekana kuwa na uzito kutokana na kila mmoja kujiandaa vizuri na vilivyo kwenye mechi zake anazoingia kutafuta alama tatu.
Liverpool na Man City wamerejesha upinzani wao kuelekea kutafuta alama zitakazowawezesha kuondoka na ubingwa huo. Hata katika mwisho wa wiki huu wameonesha nafasi yao kwenye hili kwa kuondoka na alama zao tatu kama ilivyo kawaida yao wababe hao ambao msimu huu wanaonekana kuwa vizuri zaidi.
Mashabiki wa soka duniani kote wanashangilia mtanange huu wa wawili hao japo ni kitu kinachowaumiza mashabiki wa timu hizo kutokana na hali inayoendelea na ushindani ulivyo mkubwa. Ni kipindi kigumu kwa wawili hao na kinahitaji utulivu wa aina yake ili kufanikisha safari yao ya ubingwa.
Ushindani huo haukuonekana kabisa mwanzoni mwa ligi, lakini ilipochanganya na kufikia katikati kwenye mzunguko wa kwanza harakati za kusaka ubingwa huo ziliongeza kasi yake na kufanya ligi kuwa ngumu zaidi. Jambo hilo limewaondoa Chelsea na Spurs kwenye ushindani huo na kuwaacha wawili hao waendelee kupambana kileleni.
Upande wa pili kuna safari kubwa ya upinzani kati ya Manchester United na Arsenal ambao wapo kwenye vita nzito ya nafasi ya nne na tatu; huku Spurs naye akiwa amejijumuisha kwenye kundi hilo baada ya kushindwa kutetea nafasi yake hiyo aliyoishikilia kwa msimu mzima wa kwanza na sasa amemuachia Arsenal akalie nafasi ya tatu.
Hata wakati wa Christmas ile tofauti ya alama kumi [10] iliyokuwepo kati ya Liverpool na Man City ilikuwa ni uthibitisho wa kutosha kwamba Liverpool tayari alikuwa amepata nafasi ya kusonga mbele zaidi kwenye ligi hiyo na angeweza kuchukua kombe bila ukakasi wowote lakini baadaye wakapotea kabisa na kuwaachia upenyo City ambao wanafanya kazi ya kuwasumbua kwa sasa na kuwapa vuguvugu kwenye nafasi hiyo.
Hadi sasa kumebakiwa na michezo kadhaa tu ili kuhitimisha ligi hiyo. Na hapa tutaangazia michezo ambayo wawili hawa wamesaliwa nayo na nafasi kubwa ya kuchomoka na ubingwa. Aprili 5: Southampton atamkaribisha Liverpool, Aprili 14: Liverpool atapambana na Chelsea mchezo ambao ni mgumu sana kwake, April 21: Cardiff City atapambana na Liverpool, April 26: Liverpool atakuwa na Huddersfield, Mei 4 Newcastle United v Liverpool na mwisho itakua Mei 12: kati ya Wolves watakaokaribishwa na Liverpool.
Kwa takwimu hizo tu za awali bado kuna ugumu kujua nani ataibuka kidedea kwenye mechi hizo chache zilizobaki lakini mambo yanabadilika wakati wowote kwa sababu kupoteza kwa mmoja kunampa nafasi mwingine. Hiyo ni upande wa Liverpool pekee!


Furahav
Hatari sana.