Nyota Kylian Mbappe, ambaye ana miaka 20 anafurahia msimu wake bomba pale PSG akiwa amefunga magoli 31 kwenye gemu 35 za michuano yote klabuni hapo. Pele anasema nyota huyu hahitaji kusepa klabuni hapo ili aweze kuwa mchezaji bora zaidi duniani.
Staa huyu ambaye amekuwa kwenye fomu nzuri, amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid mara kadhaa. Kinda huyu ni mmoja kati ya vijana wanaotarajiwa kuwa na kesho bora zaidi katika kazi yao ya soka la kulipwa. Kwa Pele, Mbappe anaweza kubamba na kuwa mchezaji bora zaidi duniani hata bila kuondoka klabuni hapo.
Pele, ambaye pia amekuwa akichukuliwa kama mchezaji bora wa wakati wote anamuona Mbappe kwa jicho la tofauti akiamini atakuwa mchezaji bora hapo hapo PSG ikiwa tu ataendeleza kucheza kwa ubora alio nao au zaidi.
Mbappe alikuwa ni mmoja wa vijana walioisaidia timu ya taifa ya Ufaransa kuutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2018 pia akichangia mafanikio ya kutwaa mataji mawili ya Ligue 1 na Coupe de France.
Mbappe anasifika kwa kuwa mshambuliaji mwenye utashi mkubwa, ambaye yupo shapu na mwenye uwezo wa kubadilika kubadilika.


Isaya massawe
Angeondoka psg ingekua poa pia ingemsaidia kusonga mbele zaidi