Pogba Hatii Kazi Ipasavyo United?

Pogba alirejea vyema kabisa baada ya ujio wa Ole Gunnar kama meneja wa mda kabla hajapewa mkataba kama meneja kudumu klabuni hapo. Manchester United wamepoteza gemu nyingine dhidi ya Wolves huku staa huyu akiwa hajaona nyavu kwenye gemu 7 za hivi karibuni kwa michuano yote.

Baadhi ya wadau wanahoji kama Pogba amepoteana kidogo kwenye gemu za hivi karibuni huku wakifikiria huenda ikawa ni ishu kubwa ambayo meneja wa Ole Gunnar angekuwa anaiangazia. Gunnar alikuwa na mchango wa kumrejesha kwa kasi staa huyu akifunga magoli 8 kwenye gemu 12 chini yake.

Man United walijikuta wakipokea kichapo wakiwa na wachezaji 10 dimbani baada ya Ashley Young kulimwa kadi nyekundu. Licha ya Manchester United kufurukuta, nafuu ya mchezaji mmoja kwa Wolves iliwaacha United wakipoteza pinti 3.

Ole Gunnar kwa upande wake anaona kipimo cha kufanya vizuri kwa Pogba hakiwezi kuwa magoli pekee bali mchango wa magoli anaoutoa kwa wenzake na juhudi zake za jumla za kuinua timu. Kwa mujibu wa Ole Gunnar staa huyu anafanya kazi kwa juhudi mno wakiwa dimbani japokuwa.

Hii haikuwa siku ya bahati kwa United wakipoteza pointi 3, huku meneja huyu akiacha kumtupia lawama Ashley Young kwa kadi nyekundu ambayo aliipata, anaamini Young aliamini maamuzi yake kuwania mpira yasingemletea kadi nyingine ya njano.

Acha ujumbe