Lionel Messi ameendelea kuwa na rekodi bomba ya soka baada ya kufikisha idadi kubwa zai9di ya magoli katika ligi kubwa 5 za ulaya. Messi ameingia kwenye rekodi na kuwa mbele ya Ronaldo baada ya kuchapa bao kwenye gemu dhidi ya Villarreal.
Ukiacha kuwapa ushindi Barcelona, mtata huyu alirekodi magoli yake 415, mbele ya Ronaldo mwenye jumla ya Magoli 414. Kwa hesabu za kawaida Leo amempita kwa tofauti ya goli moja tu! Lakini kwa heseabu zaidi, ukifananisha idadi ya gemu ambazo Messi na Ronaldp wamecheza na kupata magoli hayo basi Leo anakuwa mbele zaidi.
Messi amecheza gemu chache zaidi ambazo ni 446 na kupata idadi ya magoli 416 kwa mechi hizo, wakati Ronaldo yeye amepata magoli 414 kwenye gemu 514 akiwa ana gemu 68 zaidi.
Meneja wa Barcelona, Ernesto Valverde ameweka wazi kuwa klabu hiyo inamtegemea zaidi staa huyu licha ya ukweli kuwa kama staa huyu akikosekana uwanjani bado klabu hii inaweza kujaribu kucheza na kutafuta ushindi.
Gabriel
CR 7 mkal sana 👍