Klabu inapomhitaji mchezaji fulani ni dalili nzuri kwamba mchezaji husika ana thamani kubwa na ana kitu cha pekee ambacho wao wamekiona kinaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chao kwa wakati wowote ule wa huduma kutoka kwake; hivyo hufanya hivyo wakiwa na lengo mahsus.
Usajili wa wachezaji huwa na malengo ya ama kuweka sawa sehemu iliyokuwa na mapungufu katika kikosi au umri wa mchezaji aliyekuwa anacheza namba husika kufikia umri ambao hauwezi kufanya majukumu mazito ambayo kikosi kitayahitaji ikiwa kama sehemu ya kutafuta mafanikio yake.
Ikiwa ni hatua ya maandalizi, Barcelona wameweka mezani idadi ya wachezaji ambao itawahitaji ikiwa kama mbadala wa Luis Suarez ambaye kwa sasa umri wake umesogea. Hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa kwa klabu hiyo kufuatilia watu watakaoziba kabisa pengo litakaloachwa na mchezaji huyo.
Nyota huyo kwa sasa amekuwa mtu mhimu sana hata kwa kikosi cha United kutokana na kuwa na uwezo wa pekee kwa kuisaidia klabu yake iliyomlea na kumkuza kisoka hadi kuonekana mbele ya macho ya wengine kuwa ni zaidi ya bora na anafaa kuaminiwa kupewa mikoba ya mtu mwingine kwenye klabu kubwa.
Kwa maneno mengine tunaweza kusema Rashford amekuwa kisoka kwa sasa na atakuwa tishio kwa siku za mbeleni kutokana na kiwango chake alichonacho na anachozidi kukionesha kwa umri wake. Kuweza kuhusishwa na Barcelona ni hatua kubwa kwake katika mafanikio ya kisoka na anapaswa kukaza zaidi ili kujiweka sokoni.
Barcelona wamejiandaa tayari kumsajili mchezaji huyo msimu ujao endapo wataweza kukubaliana na klabu inayommiliki mchezaji huyo japo ni jaribio gumu kwa Barcelona kutokana na klabu hiyo kuuthamini kwa namna ya pekee mchango wa mchezaji huyo kwa namna ya pekee wakimpa nafasi akiwa kama mtoto wa nyumbani waliyemlea.
Matajiri hao hawajarusha jicho lao upande huo pekee kwani wametega upande mwingine wa Ujerumani kwa nyota wa klabu ya Eintracht Frankfurt anayefahamika kwa jina la Luka Jović wakiamini endapo watakosa upande mmoja basi upande mwingine utawabeba wao kutokuyumba kwenye soko hilo la msimu ujao.
Jicho jingine limeangaziwa katika klabu ya Atletico Madrid ambako walionesha nia ya kumsajili nyota wa klabu hiyo, Antonie Griezman. Japo nyota huyo alionekana kutoridhika na kujiunga na upande huo wa pili lakini wao kama klabu bado wanaendelea kumhusisha kwa kuhitaji kumfanya mchezaji wao. Kikubwa kwao ni kuzidisha ushawishi kwa mchezaji huyo.


Furahav
Suarez yuko vizuri.
Povel tz
Noma sana