Inapotokea mchezaji anafanya vizuri hupewa hadhi yake anayostahili kwa mazuri anayoyafanya na kuonekana mbele za watu kwamba ni jambo kubwa na la pekee anafanya. Nafasi hiyo hutokana na mchango anaoutoa mchezaji husika ndani ya kikosi chake na matunda yanayotokana na uwepo wake na nafasi yake kuonekana wakati akiwa hayupo kwenye mechi.
Haya yametokea tayari kwa nyota wa klabu ya Chelsea, Hazard ambaye kutokana na mchango wake tayari watu wameanza kuuthamini na kumuona kuwa ni mkongwe wa klabu hiyo. Maneno hayo yametamkwa na aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo na nyota wa zamani wa klabu hiyo, Drogba akiamini kwamba Hazard amefikia tayari heshima hiyo na anastahili kabisa kupewa heshima yake kama mkongwe.
Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa na taarifa mbalimbali zinazomuonesha kwamba anataka kutimkia Madrid ili ajiunge nao na kusakata soka la ukanda huo. Sababu nzima ya Madrid kumuhitaji ni kutokana na mchango wake wa wazi kwa klabu aliyopo na uwezo wake kuwa juu sana na unaoonekana kukua kadri siku zinavyosonga.
Maisha yake ya soka yalianzia pale Ufaransa katika klabu ya Lille ambapo thamani yake ilianza kutambulika kwenye ulimwengu wa soka na kwamba anachokifanya ni kikubwa na cha pekee, jambo lililopelekea mchezaji huyo kuonekana kwamba atafaa kwenye harakati za baadaye ndani ya klabu ya Chelsea pale walipomsajili mwaka 2012 kwa ada ya £32m.
Hadi sasa kwa muda aliopata kuwa kikosini hapo amecheza jumla ya mechi 339 akiwa kama mchezaji wa Chelsea na katika mechi zake hizo tayari amefikisha magoli 105 ndani ya klabu hiyo. Ni uwiano mzuri sana wa magoli kwa mchezaji kama Hazard kufikia. Na ni sehemu ya historia kubwa sana kwake.
Hajaweza kuishia kucheza tu idadi hiyo ya mechi na kufunga magoli hayo pekee. Pia, ameweza kutwaa vikombe akiwa na klabu hake hiyo ambapo mara nyingi mataji kama hayo huwa ndiyo heshima kwa mchezajj yeyote anapochukua mataji. Kwake ametwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili, kombe la Europa, kombe la FA na kombe la ligi.
Akizungumza na wanahabari nyota mwenzake aliyewahi kuhudumu kikosini hapo, Drogba anasema uwezo wa Hazard tayari umeshaandikwa kwenye vitabu vya klabu hiyo na ni suala ambalo nyota huyo anastahili kabisa kutokana na mchango wake aliouonesha klabuni hapo. Na anastahili kabisa nafasi hiyo adhimu kama mkongwe.
Wakati mwingine sifa kama hizi huchangia mchezaji kushuka kiwango chake cha awali kutokana na kuridhika kwamba ana upekee ambao wengi wanamwona kwamba anao. Hivyo, ili azidi kujijengea heshima hana budi kujiimarisha na kuendelea kuijenga historia yake ili kuonekana zaidi ya alipo.
Furahav
Harzad namkubali sana.