Nyota wa Real Madrid Luka Modric amefikisha idadi ya gemu 300 klabuni hapo. Modric ameshinda mataji 4 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa klabuni hapo, pia ameshinda mataji 3 ya European Super Cup, taji 1 la Spanish Championship, mataji 4 ya Klabu ya Dunia, na mataji mawili ya Super Cups kwa kipindi chote alichokuwepo na Real Madrid.
Staa huyu ametimiza idadi hii ya mechi lakini anasema bado anahitaji kuchea gemu zingine 100 zaidi. Aliingia klabuni Real Madrid mwaka 2012 na bado ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2020 huku kukiwa na mazungumzo ya kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2021.
“Imekuwa ni kipindi kirefu. Ni ngumu kusema nimebadilika, lakini nimeimarika zaidi katika kila kipengele, kama mchezaji na kama binadamu. Unachokipata Real Madrid hauwezi kukipata kwenye klabu nyingine yeyote, hii imenisaidia mimi kujiboresha zaidi. Ninafuraha na ninajivunia kuwa hapa kama ilivyokuwa siku yangu ya kwanza.”
-Luka Modric akijivunia kuwepo Real Madrid

Nyota huyu amecheza gemu zote katika kipindi cha misimu 7 toka alipoingia klabuni hapo. Anakuwa Mkroatia wa kwanza kuichezea Real Madrid gemu nyingi zaidi.


Furahav
Hongera yake.
Povel
Congratulations 🎉🤩🎉 mwamba