Lukaku Naye Anaota Kukipiga Serie A

Nyota mwa Manchester United, Romelu Lukaku ameweka bayana kuwa ni ndoto kuwa kweli siku moja akicheza soka kwenye Ligi ya Italia -Serie A!

Staa huyu raia wa Ubelgiji aliamua kuachana na soka la nchini humo na kusepea Uingereza mwaka 2011 akiwa kijana kabisa. Alichezea timu za Chelsea na Everton pia alienda kwa mkopo kule West Bromwich Albion kabla ya kwenda Manchester United mwaka 2017.

Staa huyu mwenye miaka 25 sasa, anasema katika siku za usoni angetamani kucheza soka katika Ligi ya Italia. Anatamani mno kupata nafasi kwenda kujijaribu huko. Lakini kwa sasa nyota huyu anasema anafikiria hatma yake pale Old Traffod.

“Kucheza Serie A ni ndoto, itakuwa ndoto kweli kweli. Natumaini nitaweza kucheza mapema au baadaye japokuwa kwa sasa akili yangu yote ipo Manchester United.” -Romelu Lukaku

Msimu huu Lukaku ameweza kucheka na nyavuy mara 15 kwa michuano yote.

3 Komentara

    ametisha sana

    Jibu

    Ucjal utaenda tu.

    Jibu

    Haende kila la kheri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.