Madrid Watamnunulia Nyumba Hazard

Hazard ameripotiwa kuwa amepata dili la pesa ndefu klabuni Real Madrid ili waweze kumnasa vyema staa huyu. Klabu hii ipo radhi kumnunulia nyumba ya kifahari staa huyu ili waweze kufanikiwa kuinasa sahihi ya nyota huyu.

Staa huyu wa Chelsea anaendelea kuhusishwa zaidi na klabu ya Real Madrid wakati mkaytaba wake klabuni Chelsea ukielekea ukingoni.

Hazard amekuwa akiweka wazi mapenzi yake na klabu ya Real Madrid licha ya kudai kuwa bado ana furaha klabuni Chelsea.

Lakini kwa mujibu wa chanzo cha habari cha the Sun, Real Madrid wako tayari kumnyakua nyota huyu kwa kumpa dili kabambe ambalo hatatamani kulikataa.

Ukiacha suala la nyumba ya kifahari ambayo Real wanataka iwe moja ya motisha, nyota huyu pia anaweza kupokea paundi laki 4 kwa wiki na bonasi ya paundi milioni 15 zaidi.

Staa huyu anaweza kusepa Chelsea msimu unaokuja wa joto kama Real watakubali dau la paundi milioni 100. Hata hivyo, wawakilishi wa Hazard wanadaiwa kuwa tayari wameshafanya makubaliano na klabu yake ya sasa kuhusu kuendelea kuwepo klabuni hapo.

2 Komentara

    Litakuwa dili zuri sana hazard akienda Madrid ni habari nzuri Sana kwake pia ni klabu kubwa Sana na hanaweza kuziba pengo la cr 7

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.