KUMEKUWA na stori za Paul Pogba juu maisha yake katika kikosi cha Ole Gunnar kutokana na taarifa zinazofukuta kikosini hapo kuhusu mahitaji ya nyota huyo na aina za klabu zinazotumia muda wao mwingi kutamani kufanya kazi na nyota huyo. Tangu arejee kikosini hapo kutoka Juventus ameendelea kushikilia kiwango kile kile japo wengi hawakuamini kama angekuwa na kiwango ambacho alikionesha nje ya klabu hiyo.
Uhamisho wake kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani uligharimu takriban €110M. Pamoja na fununu hizo anabaki kwenye mioyo ya wapenzi wa Manchester United kutokana na makubwa anayoyafanya uwanjani mbele yao. Uwezo wake wa kuchezesha timu na kufumania nyavu kwa nafasi yake bado unabaki kuwa kitu cha pekee kwa mashabiki.
Alionekana ni kiungo msumbufu kwenye maisha ya soka ya mwalimu Jose Mourinho baada ya kukosoa mifumo ya mwalimu huyo na kuona kwamba mfumo wake wa 4-2-3-1 haukuwa na nguvu yoyote kikosini hapo na kupendekeza mfumo wa 4-3-3 kuona kama unawafaa ndipo kuonekana hafai kabisa kwa kocha huyo na kusababisha migongano. Lakini jipya linaloendelea kwa sasa ni juu ya nani ana nafasi ya kuziba pengo lake endapo ataamua kutemana na klabu yake hiyo na kutimkia Hispania?
Toni Kroos
Jambo hili kama likitokea litakuwa ni biashara nzuri sana na yenye manufaa baina ya wawili hao, hili linatokana na kile kilichopo baina ya matajiri hao wawili kukaa na kuona kama biashara inaweza kuwa na manufaa kwa vikosi vyao. Kwa uwezo wa nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich hakuna linaloshindikana kwake lakini ni lazima upande wa Madrid uonelee kama wana deni la kupeleka mtu mwenye wasifu mkubwa kikosini hapo kwa sasa.

Adrien Rabiot
Miongoni mwa majina hatari ya viungo ndani ya kikosi cha PSG jina la nyota huyu haliwezi kusahaulika. Pamoja na kukosa mechi za kucheza msimu huu kutokana na mitafaruku ya ndani ya klabu lakini bado anabaki kuwa juu kwa nafasi yake. Hivyo, endapo Pogba kweli akaridhia kuondoka na makubaliano yakaridhiwa; biashara ya Edwoodward itakuwa haina hasara kwa sababu atatumia pesa ndogo ya mauzo kufanya usajili.
Sergej Milinković-Savić
Lazio wanajivunia sana kuwa na kiungo wa aina hii ambaye anatambua majukumu yake kikosini. Raia huyo wa Serbia, katika umri wake wa miaka 23 tu, ameweza kufanya makubwa na kikosi cha Serbia na kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa. Kutokana na uhitaji wa viungo wenye kuelewa nia halisi ya kikosi basi huyu anaweza kufanya kazi ya pekee ndani ya kikosi hicho.


devotha
pogba hawezi kuondoka man united kwa sasa yeye ndio furaha ya mashabiki
Povel tz
Gud news