Tupe Maoni ya Kikosi cha Mwaka…

Ligi kuu ya Uingereza huwa na kawaida ya kuchagua idadi ya nyota wanaofanya vizuri na kuwaweka katika kikosi cha pamoja ili kuunda timu ya msimu ya wachezaji wanaoshiriki ligi nchini humo. Timu hiyo hupewa jina la PFA Team of the Year. Hiyo huwa kama heshima na kutambua mchango wao. Baadhi ya nyota ambao kwa nafasi yetu wanaweza kuwa katika timu hiyo ni hawa wafuatao. Tukianza na safu ya ulinzi:

Ederson, mlinda mlango anayekipiga na klabu ya Manchester City ameweza kuingia katika nafasi hiyo huku akiwa bado na upinzani mkubwa kutoka kwa Mbrazil mwenzake anayekipiga katika klabu ya Liverpool, Allison. Wawili hao wamekuwa na msimu wa pekee sana japo chaguo letu la kwanza ni nyota huyo.

Trent Alexander-Arnold, ameweza kufanya kazi ya pekee sana akiwa katika safu ya ulinzi kwenye kikosi hicho. Nafasi yake ni kubwa sana na haijaonekana kuwa na mapungufu makubwa, katika umri wake anastahili kabisa kuwa katika nafasi hiyo.

Andy Robertson, mlinzi mwingine wa Liverpool ambaye ameweza kuwa na kiwango cha aina yake ndani ya kikosi hicho. Ni aina ya walinzi wa kileo ambao wanapandisha mashambulizi kwa kasi na kurudi kwa haraka kuzuia.

Aymeric Laporte, kwa nafasi yake ameweza kuzuia ule upenyo ambao klabu hiyo iliweza kukumbana nao kwa kipindi kirefu sana. Amekuwa mhimili kwenye matokeo ya kikosi chake hicho kwa kufanya safu yao kuonekana imara kwa wakati fulani.

Virgil van Dijk, mleta mabadiliko makubwa sana ndani ya kikosi cha Liverpool; kwa hakika yale mapungufu ya kipindi cha nyuma ndani ya kikosi hicho yameweza kufukiwa kabisa kutokana na ujio wa nyota huyo na anastahili sana kuwa ndani ya kikosi hiki.

Safu ya kiungo imesheheni nyota wengine kutoka Manchester City wakiwemo Fernandinho na Bernardo Silva, wawili hawa kwa hakika wamekuwa mhimili mkubwa sana ndani ya kikosi chao hata kuchochea nafasi yao kubwa kuelekea ubingwa msimu huu. Nafasi yao ndani ya kikosi cha ligi cha mwaka ni kubwa mno kutokana na makubwa waliyofanya.

Mbali na hao kuna nyota mwingine ambaye ingizo lake linaweza kuwashangaza wengi lakini kwa hakika ni mhimili mkubwa sana ambao umefanya makubwa ndani ya kikosi cha United naye ni Paul Pogba. Kwa nafasi fulani mchango wake umeonekana na anafaa kupewa nafasi ndani ya kikosi hicho.

Safu ya ushambuliaji imeshikwa na watu watatu ambao ni Sadio Mane, Raheem Sterling na Sergio Aguero ambao wote wamekuwa tishio kwa safu yoyote ya ulinzi ambayo wanakutana nayo na kwa hakika wanastahili heshima yao kutokana na uwezo wao mkubwa mbele ya lango wanapokubana na timu pinzani.

Makala iliyopita
Makala ijayo

4 Komentara

    Sadio Mane, Raheem Sterling na Sergio Aguero ambao wote wamekuwa tishio kwa safu yoyote ya ulinzi

    Jibu

    Hii iko poa.

    Jibu

    Raheem Sterling na Sergio Aguero ambao wote wamekuwa tishio kwa safu yoyote ya ulinzi

    Jibu

    Sadio mane ametamba sana hata akikosa katika mechi moja tu huwa timu inakosa Mouton’s

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.