Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka wazi timu sita anazozikubali, ambazo hutumia mda wake kuziangalia mara kwa mara. Katika timu alizotaja, kati ya hizo mbili ni wapinzani wake wa Ligi Kuu ya Uingereza na mabingwa wengine wa Ulaya.
Liverpool wanakutana na Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, mzunguko wa kwanza unaanzia Barcelona Jumatano.
Kabla ya kukutana na Barca, vijana wa Klopp watakuwa wenyeji wa Huddersfield dimbani Anfield usiku wa Ijumaa Oktoba 26. Kama Liverpool watashinda mexhi hii watarejea kileleni Juu ya Man City.
Jurgen Klopp anasema kuwa Manchester City ni moja ya klabu ambazo anafurahia kutazama wakicheza, klabu zingine anazozipenda ni Tottenham, Barcelona, Bremen, Dortmund na Mainz.
Meneja huyu anaamini ana kibarua kigumu kupambana na Barcelona, lakini anajipa matumaini kuwa vijana wake hawatalaza damu.

