Mara nyingi wengi hudhani kumiliki klabu ni uwekezaji mkubwa sana kutokea lakini ni biashara ambayo inahitaji akili, uwazi, kujitoa na kuchukua tahadhari kubwa sana katika utekelezaji wake. Leo tunakuletea matajiri wanaomiliki klabu na kiwango cha pesa walichonacho kwenye uwekezaji huo. Hili halitahusisha klabu zinazomilikiwa kwa hisa au kundi la watu kama ilivyo kwa Manchester City.
Shahid Khan- Fulham FC, ni mfanyabiashara mkubwa na mwenye historia kubwa sana kwenye umiliki wa klabu hiyo. Tajiri huyo mwenye asili ya Pakistani na Marekani amejenga misingi ya uwekezaji ndani ya klabu hiyo. Huku klabu yake ikiwa na utajiri wa takriban $4.1 bilioni (£2.5 bilioni). Japo suala la kwamba alitumia kiasi gani kununua klabu hiyo halikuwekwa wazi lakini inakadiriwa kuwa ni $200 milioni (£119 milioni).
Malcolm Glazer na Family – Manchester United, hawa ndiyo wanaoifanya United izidi kuonekana hivyo ilivyo kwa sasa. Pia, wanamiliki timu ya NFL pale Florida. Walikamilisha umiliki wa klabu hiyo katikati ya miaka ya 2003 na 2005. Wanakadiriwa kuwa na uwekezaji wa kiasi cha $4.1 bilioni (£2.5 bilioni).
Mike Ashley – Newcastle United, maisha yake ya umiliki yalianzia pale alipofungua duka la vifaa vya michezo na baadaye kuwa nguli kwenye masuala hayo. Ndipo alipojiingiza kabisa kwenye biashara hiyo. Anamiliki klabu hiyo akiwa tayari na utajiri wa $5.5 bilioni (£3.3 bilioni) zinazoiongoza klabu yake hiyo.
Stan Kroenke – Arsenal FC, ana utajiri kutokana na aina yake ya uwekezaji kwenye michezo. Akiwa na umiliki wa Arsenal na hisa ndogo ndogo katika klabu nyinginezo nje na Uingereza. Ikiwa ni upande wa NHL, mpira wa kikapu hata NFL. Utajiri wake ndani ya Arsenal unakadiriwa kufika $5.6 bilioni (£3.4 bilioni).
Suleiman Kerimov – Anzhi Makhachkala, hii klabu ya nyumbani kwake muwekezaji huyu wa Urusi na mwanasiasa wa taifa hilo. Mwaka 2011 aliinunua akiwa na lengo la kuigeuza kuwa klabu kubwa sana duniani. Alitumia mamilioni kuwashawishi Willian, Lacina Traore na Samuel Eto’o ili afanye nao kazi lakini alishindwa kibajeti. Utajiri wake ni $6.9 bilioni (£4.1 bilioni).
Ifeanyi Ubah – Ifeanyi Ubah FC, aliipa klabu jina lake klabu hiyo ya Nigeria akiwa anafahamika kama Ifeanyi. Alianza kufanya biashara akiwa na miaka 16 pekee akizunguka miji ya Nigeria, Ghana na Sierra Leone na taratibu akaendelea hadi Liberia; akiwa msafirishaji wa vifaa mbalimbali. Utajiri wake ni $3 bilioni (£2.4 bilioni).
Roman Abramovich – Chelsea FC, miongoni mwa wawekezaji wa Urusi waliotawala soka la Uingereza aliinunua klabu hiyo kutoka kwa Kane Bates, 2003. Baada ya hapo alifanya uwekezaji wa £700 milioni ili kuimarisha kikosi ambacho kilimpa mataji baadaye. Ndani ya uwekezaji huo amefanikiwa kutengeza yapata $9.1 bilioni (£5.5 bilioni).
Hao ni baadhi yao tu ya wengi wanaomiliki klabu na kuzigeuza klabu zao hizo kama sehemu ya biashara yao.

