Klabu ya soka inayokipiga katika ligi ya Hispania inategemewa kutua nchini Tanzania kama sehenu yao ya maandalizi ya mapema ya msimu mpya wa ligi. Baada ya ligi kukamilika mizunguko yake klabu nyingi huchukua nafasi ya kusafiri na vikosi vyao mbali kabisa na mataifa yao ili kupumzisha nyota wao na kubadili mazingira.
Mwaka huu imekuwa zamu ya Tanzania kutembelewa na ugeni wa aina hii ambapo miamba hao wa soka wanategemewa kutua nchini kwa ajili ya mapumziko hayo na wanategemewa kucheza mchezo wa kirafiki na klabu moja ambayo huenda ikawa wakongwe wa soka Tanzania kati ya klabu ya Simba au Yanga.
Kwa hakika katika historia Sevilla itakuwa ni klabu kubwa ya pili kutua Tanzania na kucheza mechi na klabu za ndani huku Everton ikiwa ni klabu ya kwanza kabisa kuingia nchini hapa na kucheza mechi ya kirafiki. Kwa mwaka huu itakuwa zamu ya klabu za ndani za nchi sio kama msimu uliopita.
Mechi hiyo inategemewa kuchezwa Mei 23 ambapo itawafanya mashabiki wa soka kushuhudia soka safi kabisa kutoka kwa klabu hiyo kongwe ya Hispania. Ni imani ya kila mmoja kwamba kwenye mechi hiyo itakayofanyika katika uwanja wa taifa itakuwa kipimo tosha cha klabu hizo kuweza kujifunza kitu kutoka wa mataifa hayo mengine.
Inakumbukwa kutua kwa Everton Tanzania hakukuweza kabisa kuwanufaisha wenyeji bali ilikuwa na faida kwa klabu ya Kenya, Gor Mahia ambayo ndiyo ilipata nafasi ya kucheza mechi na Waingereza hao. Kwa sasa nafasi ni ya wenyeji kuonesha ubora wao mbele ya wageni hao.
Wakurugenzi wa ligi hiyo wamethibitisha wazi kabisa juu ya suala la klabu hiyo inayoshiriki ligi yao kusafiri hadi Tanzania na kuwa karibu na mashabiki zao kwa kutambua uwepo wao zaidi ya kuishia kuwatazama lakini kwa awamu hii imekuwa karibu nao kwa kuwafikia kabisa.
Kutua kwa Sevilla ni jambo la kujenga na lenye uzalendo zaidi kwa kuona kwamba njia za wachezaji wetu zinaweza kufunguliwa kwa sababu nguvu ya klabu hizo za kigeni kisoka ni tofauti sana na klabu zetu za ndani. Hivyo hiyo ni sehemu ya vilabu hivyo kujifunza, kuuza majina yao na kuonesha uwezo zaidi.


Omary lukumbi
Duuh hii itakua si kirafiki tuu hata utalii pia nchini kwetu
Povel
Habar njema