“Tunataka Wachezaji Wenye Uhalisia!” – Ole

Mambo yanaendelea kuwa magumu ndani ya klabu ya Manchester United kukiwa hakuna matokeo yanayoridhisha ndani ya klabu hiyo jambo ambalo linakuwa haliendi sawa upande wa kocha kwani tangu apokee kikosi hicho kwa mkataba wa kudumu hajapata matokeo ya aina yoyote anayoweza kujivunia.

Hakuna muunganiko mzuri wa wachezaji huku baadhi wakianza kuonesha dhahiri nia zao za kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho ili kupisha klabu hiyo kuangalia aina ya nyota watakaoendana na falsafa ya klabu hiyo ili kutetea hadhi ya klabu na kuirudisha kama ilivyokuwa awali.

Hadi sasa kuna kauli zimeanza kutoka ndani ya klabu kwamba kuna baadhi ya wachezaji wanapewa upendeleo zaidi ya wengine na hata katika upangwaji kuna wachezaji wengine hawapati nafasi kutokana na uwepo wa aina hiyo ya upendeleo. Huenda mgawanyiko huo ni kitu pekee kinachoisambaratisha klabu kwa sasa.

Japo kwa kuangalia mambo kwa undani zaidi tunaweza kusema chanzo cha mapungufu ndani ya klabu hiyo ni uongozi hususan upande wa wakurugenzi, Edwoodward, ambaye kwa nafasi yake, anataka kusimamia kila idara ya kikosi kitu anbacho kinakosesha uhuru wa makocha kuchagua aina ya wachezaji wanaofaa. Lakini kutokana na hali iliyopo kwa sasa sio wakati wa kumtafuta mchawi ni nani bali ni kuangalia namna ya kurudi kwenye uhalisia ambao mapema wachezaji walikuwa wanauonesha kwa nguvu zao zote ili kupambania nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

“Tunataka Wachezaji Wenye Uhalisia!” – Ole

Kocha wa klabu hiyo hadi sasa anaona kwamba ana aina mbili za wachezaji ndani ya kikosi chake baada ya kupokea vichapo mfululizo. Anaona kabisa kuwa ana wachezaji ambao wapo tayari kujitoa kwa namna yoyote ile kupambania ushindi wa klabu yao lakini anao ambao kwao huo moyo wa kupambana hawana kabisa.

Msimu ujao wa usajili ambao kwa hakika hata kocha mwenyewe anaombea ufike haraka atakuwa na machaguo yake juu ya nani asalie klabuni na nani aendelee na maisha yake nje ya klabu. Hilo litakuwa na nguvu zaidi kwa kocha huyo kuonesha ushindani zaidi.

Kazi ngumu

Hadi sasa kimbilio lake ni kuona msimu unaisha vizuri na wanapata nafasi ya kusonga mbele zaidi kitu kikubwa kwake ni kuweza kuibuka na ushindi kwenye mechi yake na Chelsea ili angalau kufuta uteja alionao hadi sasa kwa klabu kubwa zinazoshiriki ligi hiyo.

Pia, ushindi huo unaweza kuwa ni njia ya kujua kama watapata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa katika msimu ujao au watakuwa nje ya hiyo michuano.

2 Komentara

    Duuh pole yao

    Jibu

    Ndio aina ya wachezaji watakaoipa heahima united

    Jibu

Acha ujumbe