Mashetani wekundu wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa klabuni hapo kwa kusajili damu mpya. Meneja huyu sasa ameamua kuweka bayana aina ya wachezaji ambao anatarajia kuwasajili kwenye dirisha la usajili kiangazi.
United wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kibao msimu huu, ambao wanadaiwa watatimba klabuni hapo msimu wa joto, wapo wanaotajwa kuwa na mpango wa kusepa klabuni hapo pia. Safu ya ulinzi ya klabu hiyo ni moja ya sehemu muhimu inayoangaliwa zaidi katika maboresho ya kikosi.
Solskjaer anatambua vyema changamoto ya usajili kwa miaka hii ukilinganisha na miaka ya 1990 na 2000 iliyopita. Meneja huyu ansema kuwa pesa imeakuwa ndiyo kila kitu kwa sasa, wakati ambao wachezaji wanavutiwa na dau zaidi.
Meneja huyu wa United anasema kkwa sasa hawahihitaji wachezaji wa aina ya kuangalia dau zaidi au nafasi zao. Ole Gunnar anasema, wao watazingatia zaidi ubora wa wachezaji.
Umaarufu na pesa vimekuwa vikiwaendesha zaidi wachezaji, Ole Gunnar anasema wachezaji wa aina hii siyo wachezaji sahihi kwa klabu ya Man United.
Wachezaji ambao wamekuwa wakihusishwa na klabu ya Manchester United ni pamoja na Kalidou Kouliblay wa Napoli, Nicklas Sule wa Bayern Munich kwenye safu ya ulinzi. Wengine wanaotajwa kuwa wapo kwenye mpango wa mabadiliko makubwa ya kikosi ni Chris Smalling, Phil Jones na Eric Bailly ambao huenda wakapoteza nafasi zao.


Nasra
Wachezaji wa mm man U wanaushirikiano sana