Sifa Apewe Messi au Valverde!

Wote wawili wamekuwa muhimu katika mafanikio ya Barcelona msimu huu, huku messi akiwa na uzoefu mkubwa zaidi klabuni hapo. Wadau wanajiuliza nani anastahili sifa za pekee baada ya Barcekona kuinua taji jingine la La Liga kwa msimu wa mwaka 2018-2019.

Barcelona wameshinda taji hili kwa mara ya 8 katika misimu 11 Messi akiwepo klabuni hapo na kupeta Hispania, na ulaya kwa ujumla. Kwa ujumla wametwaa mataji 26 ya La Liga.

Valverde Anasemaje?

Valverde amekuwa ni msiri sana wa mipango yake, akidaiwa kuwa mara nyingi haweki wazi sana mipango yake kwa ujumla. Mchango wake ni mkubwa mno klabuni hapo. Kama mameneja wengine, uhusiano mzuri kati yake na Messi umekuwa muhimu sana kwa ushindi wa klabu hii.

Valverde anatambua mchango mkubwa wa Messi toka anafika klabuni hapo, ambaye kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kuwa wa moto licha ya umri kuanza kumtupa mkono.

“Messi ndiye kiini cha haya yote. Mda alioutumia Barcelona, pamoja na kipindi chote kulipokuwa na makocha tofauti, wakati wa Leo Messi amefanya makubwa mno. ” -Valverde akimsifia Messi

Mameneja karibu wote wa kipindi cha Messi wamekuwa wakiwekeza sana kwenye furaha ya mchezaji huyo kama motisha ya kufanya vizuri zaidi na kuendelea kusalia klabuni hapo.

“Tunatakiwa tuwe wakweli kuwa amekuwa mchezaji bora wa dunia kwa wakati wote. Tumekuwa tukimfurahia kila wakati akicheza, tunatakiwa kujivunia kwa ubora alionao.” Luis Suarez

Kifuatacho

Barcelona wanatarajia kushinda mataji matatu kama watatoboa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Hii itamfanya Valverde aingie kwenye vitavu vya Historia vya klabu hiyo.

2 Komentara

    Ahsante kwa taarifa #meridianbettz

    Jibu

    asante kwa ujumbe wenu

    Jibu

Acha ujumbe