Umtiti Kutimba Old Trafford

Nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa na mlinzi wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti ameweka wazi hisia zake kwa baadhi ya nyota kwa kuwaambia hali halisi inaweza kumfanya atimke klabuni hapo wakati wowote ule. Tayari ameshaandaa mahali pa kutua muda wake ukifika kutokana na kushuka kwa mapendeleo ya kocha Valverde kwake.

Messi ni baadhi ya nyota ambao Umtiti amewaambia jambo lake hilo, pia, nyota wengine wamepewa taarifa na mchezaji huyo juu ya safari yake mpya hiyo ndani ya jiji la Uingereza. Nyota huyo pamoja na uwezo wake amepoteza kabisa nafasi ya ushiriki ndani ya kikosi chake kwa sasa.

Mlinzi huyo wa klabu hiyo ameliona suala lake la kukosa muda wa kucheza kikosini hapo ndilo sababu kubwa ya yeye kuondoka na baadhi ya watu muhimu ndani ya kikosi hicho kama Gerald Pique na Messi wameshataarifiwa na mchezaji huyo kwamba hatamani kuendelea kusalia hapo kwa msimu mwingine.

Taarifa hizo siyo rahisi hata kwa United kuzizuia kutokana na uhitaji wao wa mlinzi wa kati baada ya kukosa nyota ambaye anaweza kufanya kazi kama ile inayofanywa la nyota wa klabu hiyo, Victor hivyo endapo lengo lake hilo litatimia basi atapata nafasi ya kutimkia Uingereza.

Kitu kingine mbali na kukosa nafasi ya kucheza ndani ya klabu yake hiyo, pia, nyota huyo amekwenda mbali sana na kuangalia kwamba nafasi yake ya kucheza ndani ya kikosi cha Ufaransa ni kama atakuwa na muda mwingi wa kuonesha uwezo wake ila hali yake ikiendelea vile basi ni ndoto kwake kuchezea taifa lake.

Kwa sasa ni kivuli cha Pique na Lenglet katika safu nzima ya ulinzi ya klabu hiyo ya Barcelona lakini uzito wa nafasi hiyo unakuja kutokana na taarifa zinazoendelea kwamba klabu hiyo ipo katika mipango ya kumsajili mlinzi wa Ajax, De Ligt. Kama nyota huyo atatua hakika atakosa kabisa namba!

Hadi sasa United wanaonekana kulifutilia mbali tamko lao la kumsajili Coutinho na kuamua kuwekeza nguvu zao katika safu ya ulinzi kwanza ikiwa nyota huyo ni miongoni mwa walinzi wenye uwezo wa juu japo anakosa namba ya kudumu na ndani yake amejijenga katika majukumu binafsi ya kuwa bora zaidi.

Kwa nafasi fulani uwepo wa Umtiti, Lindelof, Rojo na Bailly unaweza kuwa na kitu cha kipekee kikosini hapo maana ni aina ya walinzi wanaojiamini katika maamuzi yao na uwezo wao sio wa kubeza kabisa wakiwa uwanjani.

Uzuri wa Umtiti ni aina ya walinzi wenye utulivu hata wakati wa kutoa pasi au kushambulia hivyo kutokana na mabadiliko ya kisoka kwa karne hii itasaidia sana kuijenga timu hiyo upya.

3 Komentara

    Safi

    Jibu

    Vizur inapendeza

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.