Utawala Mpya Newcastle…

Kuna taarifa zinashika kasi kwamba klabu ya Newcatle ipo hatihati kupoteza umiliki wa awali na kuachia utawala mpya ambao upo katika mazungumzo ya mwisho na kuna kila dalili ya kuuziana klabu hiyo na tajiri mkubwa kutoka nchi za Kiarabu, tajiri huyo anahitaji umiliki wa kuiendesha klabu hiyo.

Kama wataweza kukubaliana ndani ya klabu hiyo kunahitajika kusuka mizizi na mfumo mpya ili kuonesha ufanisi mkubwa na umewafanya kuvutiwa na kuona klabu hiyo inaweza kufika mbali na kupata mafanikio ya kila aina.

Bilionea, Shekh Khaled Bin Zayed na kundi lake zima la Abu Dhabi ndiyo wanaotaka umiliki wa klabu hiyo na wapo tayari kutoa fungu nono la pesa kwa Ashley ambaye ndiye anaishikilia klabu hiyo kwa sasa bila tatizo lolote. Naye Ashley hajaonesha nia ya kukataa kuiuza klabu hiyo na kuachana na uwekezaji hapo.

Utawala Mpya Newcastle…

Miongoni mwa matumaini makubwa ya bilionea huyo ni kusuka utawala na uongozi wa aina yake ili kuifanya Newcastle kuwa yenye ushindani wa aina yake. Tayari ameweka jicho lake kwamba atatamani sana katika uundaji wake wa kikosi aweze kuwa na watu aidha Mourinho au Wenger ili waweze kuishikilia klabu yake hiyo.

Ni ndoto yake ya nuda mrefu kumiliki klabu ya soka na anaona kabisa suala hilo linakwenda kufanikiwa kwa sasa kwa asilimia nyingi sana. Na hana wasiwasi juu ya hilo lakini kwa upande mwingine kipenzi kikubwa cha mashabiki, Benitez atakuwa nje ya kikosi chake hicho endapo mambo yatakwenda hivyo.

Kuna uwezekano biashara hiyo ikafanyika na kiwango cha £350M kimeandaliwa ili kushawishi mmiliki wa awali, Ashley aweze kuachana na umiliki wake wa awali wa klabu hiyo jambo ambalo linaonekana kutokuwa na upinzani kabisa kwa tajiri huyo kuelewana na bilionea huyo.

Hofu yake ni kwa mashabiki zake ambao wamempa nguvu kwa miaka mingi tangu awe na klabu hiyo na jingine ni vile alivyokuwa karibu na mwalimu Benitez na kwamba kwa sasa watakuwa mbali naye na anaonekana kusitisha hata makubaliano ya mkataba maana hali ya umiliki inaelekea mikononi kwa watu wengine.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.