Wababe wa UEFA Kukutana Super Cup

Kwa mara ya kwanza katika historia klabu mbili kutoka Uingereza ziataumana ndani ya kombe hilo kubwa sana kwenye historia ambalo hukutanisha washindi wa vikombe viwili vya UEFA jambo ambalo huwa la kihistoria na aina hiyo ya mechi mara nyingi huwa nzuri na yenye kuvutia kwa kiwango kikubwa.

Chelsea yeye ni bingwa wa UEFA Europa ambayo alijinyakulia baada ya kumpa dozi ya pekee Arsenal ndani ya ligi hiyo ambayo wawili hao walikutanishwa kule Baku. Huku Chelsea wakionesha kabumbu kali na la pekee sana ambalo lillwafanya vijana wa Unai wasifue dafu mbele ya Sarri.

Mechi hiyo nayo iliacha historia kubwa kwenye ramani ya soka huku wawili hao kutoka Uingereza walipokutana kuziumiza nyasi. Katika mechi hiyo baadhi ya wakongwe wa klabu hizo waliaga baada ya kutumikia klabu zao kwa mafanikio makubwa na ukiwa ni wakati wa wao kujiengua na kuwaachia wenye damu changa.

Upande wa pili, Liverpool wanapata nafasi ya kuingia ndani ya kikombe hicho baada ya kuwa na msimu wa ajabu kwa kuwafunga Tottenham kwenye fainali ya klabu bingwa Ulaya. Hayo ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo na kocha ambaye hana misimu mingi kikosini, Klopp.

Mechi ya wawili hao ilikuwa ya kihistoria baada ya miaka mingi klabu kutoka Uingereza kuwa katika kiwango kibovu sana na kuachia klabu mbili za Hispania kutawala sana soka hilo. Wanasema wakati ni kama ukuta kauli hiyo imepotea kabisa na sasa ile heshima imerejea upya Uingereza.

Kwa historia ya klabu hizi mbili japo Liverpool atapigiwa sana upatu kutokana na kikosi chake lakini kwa hakika mechi yao ni ngumu sana kutokana na aina ya kikombe wanachokwenda kupigania wawili hao. Ni kikombe chenye thamani kubwa hivyo lazima ugumu ndani ya mechi hiyo uonekane.

Liverpool anaweza kujihami kwamba kikosi chake kimewafunga vigogo wengi Ulaya msimu huu lakini mara nyingi klabu za ukanda mmoja zikikutana hufanya mechi kuwa ngumu sana kutokana na aina ya upinzani uliopo na namna walivyokwisha zoeana ndani ya ligi yao ambapo hukutana mara kwa mara.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Agosti 14, 2019 huku tukishuhudia wababe hao wakiumana uwanjani kutetea heshima zao baada ya kuwa na mafanikio ya kipekee sana kuzidi wengine.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.