Baada ya bodi ya FIFA kukaa miezi kadhaa iliyopita walipendekeza baadhi ya marekebisho ya sheria zenye nia ya kuboresha soka na kulifanya liwe ni lenye mvuto mkubwa sana mbali na hivi ilivyo sasa. Kanuni hizo hazina athari kubwa sana ndani ya soka ila zinatengeneza baadhi ya uhuru kwa wachezaji.
Mabadiliko hayo yalifanywa katika kipindi cha Rais wa FIFA, Infantino ambaye kwa mara nyingine amepata nafasi ya kuongoza shirikisho hilo hadi itakapofika 2023 kutokana na mchango wake ndani ya soka na makubwa ambayo wengi wameridhika na utendaji kazi wake kwa kipindi kilichopita.
Amepita bila kupingwa na yeyote na sasa itakuwa ni wakati wake kuona yale ambayo ameyaweka katika maandishi yakifanya kazi. Baada ya kuona utendaji kazi wake atakuwa amejijengea historia ya pekee sana ndani ya shirikisho hilo na kwa vizazi vijavyo vya soka. Baadhi ya vitu vilivyofanyiwa marekebisho ni:
Endapo penati imeokolewa au mpira umegonga mwamba na kurudi uwanjani hakuna mchezaji anayeruhusiwa kuucheza kwa mara nyingine ili kufunga goli bali mpira utarejeshwa uwanjani na kuchezwa kama kawaida na hilo litahesabika kama sio sehemu ya kuiadhibu timu husika. Hivyo hakuna haja ya wachezaji kujipanga nje ya 18 kusubiri mpira (rebound).
Goli lolote litakalokuwa limefungwa kwa mkono halitakubaliwa na kitakachoamua hapo ni mpira wa adhabu kwa sababu kulikuwa na utata katika hilo na kwamba endapo mpira umeshikwa na goli likaingia basi ilikuwa inahesabika kama goli kwa baadhi ya waamuzi hivyo kuleta utata.
Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira kutoka kwa golikipa yaani baada ya kudakwa na sio kusubiri mpira huo utolewe ndani ya eneo la 18 kama lilivyo sasa. Mchezaji atakuwa huru kuucheza mpira ambao umedakwa na mlinda mlango hata katika eneo la ndani ya 18.
Wachezaji wa upande unaopiga mipira ya adhabu (yaani mipira iliyokufa) hawataruhusiwa kusogea eneo lililopimwa na muamuzi ili kwenda kuwasumbua wale wa timu pinzani wakati mpira utakapokuwa unachezwa bali watatakiwa kukaa mbali na eneo la tukio ili kupisha wahusika kujipanga.
Mchezaji anayefanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutokea upande wowote wa uwanja ili kuepusha upotevu wa dakika.
Kocha atakuwa akipewa kadi badala ya maelekezo mengi pale atakapokuwa anavuka eneo lake la uongozi alilotengewa badala ya kumuacha apokee maonyo mengi na kurudishwa katika eneo lake kama ilivyo sasa!
Unaonaje sheria hizi?

