2019 Balaa Neymar, Anaikosa Copa America

Huu ndiyo unaweza kuwa mwaka mgumu zaidi kwa staa wa PSG na Brazili, Neymar katika kipindi chake chote cha soka la kulipwa.

Nyota huyu amekosa gemu nyingi za PSG, zikiwepo za Ligi ya Mabingwa kwa sababu ya jeraha la mguu alilolipata mwezi Januari lililomlazimu baadhi ya gemu azitazame kwa Televisheni tuu.

Brazil wamethibitisha kuwa staa huyu hataweza kucheza 2019 Copa America. Hii ni taarifa mbaya kwa nyota huyu mwenye umri wa miaka 27.

Mwezi Januari mwishoni Neymar alivunjika mguu kwenye gemu dhidi ya Strasbourg, jeraha hili lilimuweka nje ya uwanja hadi mwezi Aprili. Katika kipindi hiki alikosa mechi muhimu, moja ya mechi hizo ilikuwa ni mechi dhidi ya Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mwezi Aprili alizuiwa kucheza mechi 3 baada ya kuwatukana maofisa wa Manchester United kwenye gemu ambayo PSG walichapwa 3-1 wakiwa nyumbani.

Mwezi huo huo pia alimpiga konde shabiki aliyemtania baada ya kupoteza mechi ya fainali ya French Cup dhidi ya Rennes. Walifungwa 6-5 kwenye mikwaju ya penati, na akapewa adhabu ya mechi tatu tena.

Mwezi Mei pia umekuwa na balaa kwa nyota huyu akianzakwa kuvuliwa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil kwa sababu ya ishu ya nidhamu, nafasi iliyochukuliwa na Dani Alves.

Mwezi Juni ameuanza vibaya tena baada ya kupata jeraha jingine la enka linalomfanya aikose michuano ya Copa America. Staa huyu alianza kucheza gemu dhidi ya Qatar, lakini haikupita hata dakika 20 alipata jeraha na kutoka uwanjani akimwaga machozi.

Hakika mwaka 2019 umekuwa mwaka wa balaa kwa Neymar, bila shaka miezi iliyobakia itakuwa miezi ya heri kwake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.