Nyota wa Manchester United Paul Pogba anaendelea kutikisa vichwa vya habari za michezo kwa kuripotiwa kuwa yupo tayari kurejea Juventus. Jarida moja la Italia limechapisha kuwa ili staa huyu atue Juve wanahitaji mastaa kadhaa.
Pogba anatajwa kutokuwa na furaha kwa anavyochukuliwa pale Manchester United kuanzia klabu yenyewe, mashabiki na vyombo vya habari vinavyomzungumzia. Bila shaka ana matumaini kuwa hali hii itabadilika akienda Juventus.
Taarifa zinaripoti kuwa staa huyu amekuwa akitembelea Italia mara kwa mara, mara ya mwisho alienda kwenye sherehe ya kustaafu ya Andrea Barzagli ambayo pia ilikuwa ni sehemu ya kusherekea ubingwa wa Italia.
Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, Pogba anahitaji yuko gado kurejea Juve baada ya uhamisho wake uliopita wa paundi 105m, lakini kama staa huyu batarejea klabuni hapo basi pesa za uhamishao wake zinahitaji kutafutwa. Hivyo Juve watahitaji kuwauza Joao Cancelo, Douglas Costa, Mario Mandzukic na Mattia Perin.
Wachezaji hawa wanatarajiwa kusepa klabuni hapo kwa sababu wanatajwa kuwa hawapo kwenye mpango ya staili mpya ya Maurizio Sarri au wale wanaushuka thamani.


Gabriel
Habar njema