Aliyekuwa meneja wa Luciano Spalletti bado anawalilia klabu ya Inter Milan, anaamini kwa upande fulani klabu hiyo huenda haikumfikiria vyema kwa kuzingatia mchango wake klabuni hapo.
Spalletti anadai kuwa alipata heshima kubwa sana kuwa meneja wa klabu hiyo, licha ya kutimuliwa kwake na kibarua chake kuchukuliwa na Conte. Alipokuwa meneja amefanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa miaka 2 mfululizo.
Spalletti anadai kuwa bila shaka, atakumbuka kwa dhati kipindi chote alichokuwepo klabuni hapo. Atakumbuka pia jitihada za pamoja za kujaribu kujenga kikosi cha Inter Milan kwa kuzingatia majukumu ya watu tofauti klabuni hapo.
“Nimepata heshima kupata fursa ya kuifundisha Inter, nitakumbuka kwa dhati nyakati tulizokuwa pamoja. Katika kujaribu kujenga, klabu imehitaji baadhi ya majukumu yachukuliwe na watu fulani. Ni timu nzuri yenye mashabiki safi sana.” -Luciano Spalletti
Spalletti anakiri pia kuwa toka alipotimuliwa bado hajapata ofa kwa ajili ya msimu unaokuja, anatazamia huenda akapata ofa ya kuitumikiaklabu nyingine.


Furahav
Vizuri sana.
Povel
Duh