Aliyekuwa meneja wa Newcastle United, Rafael Benitez anatarajia kurejea Uingereza kuungana tena na klabu yake. Anasema anaweza kurejea Newcastle siku moja.
Benitez alisepa klabuni hapo Juni 20 mwaka huu baada ya kushindwa kufikia muafaka wa mkataba wake mpya na mmiliki wa Newcastle United, Mike Ashley.
Kwa sasa Benitez ni meneja wa klabu ya Uchina ya Dalian Yifang. Benitez anatarajia kurejea Uingereza baada ya kutumikia mkataba wake wa sasa wa miaka miwili na nusu.
Akihojiwa kama angependa kurejea Newcastle United baada ya kumaliza mkataba wake wa sasa, amesema; Ninatarajia kufanya vyema hapa Dalian, na kisha kurejea UK. Sijui ni lini lakini wakati wote unakuwa na furaha kurejea mahali ambapo watu wanathamini mchango wako. Mashabiki wa Necastle United wamekuwa mashabiki bora sana kwangu katika kazi yangu kama meneja.
Bwana huyu mwenye miaka 59 anawatakia Heri Newcastle United akiwaombea wafanikiwe kwa wayapangayo.


neema hassan
Asante kwa taarifa#meridianbettz