Viwanja Bora Duniani

Soka siyo tu mchezo wa kushindanisha timu mbili uwanjani, pia, linaendana na uwekezaji katika viwanja ambavyo mara nyingi huwa ni kivutio kikubwa cha mashabiki; pia, huchochea wachezaji kucheza kwa namna inayoendana na kuleta hamasa kwa wachezaji wanaotumia uwanja huo. Leo tunakuketea viwanja bora kabisa vyenye heshima kubwa duniani na vyenye muonekano mzuri:

Soccer City

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1989, ni miongoni mwa viwanja vyenye heshima kubwa duniani na unapatikana huko Johannesburg, Afrika Kusini. Kutokana na kutumika kwa muda mrefu sana, mwaka 2009 ulifanyiwa marekebisho na ukatumika kwenye kombe la dunia 2010. Una uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 100,000.

The Maracanã

Ni uwanja wenye historia kubwa sana katika taifa lenye vipaji vingi sana vya kila aina. Ulijengwa 1950 ambapo ni mwaka Brazil waliandaa fainali za kombe la dunia; inakumbukwa katika mechi hiyo Brazil walipoteza katika uwanja wao mpya mbele ya Uruguay.

The Allianz Arena

Ulifunguliwa mwaka 2005 ikiwa ni sehemu ya viwanja vyenye historia kubwa hadi sasa. Uwanja huu umetengenezwa kwa teknolojia kubwa kwani una uwezo wa kubadili rangi zake kwa namna inavyopendezwa kuwa. Hutumika na klabu mbili za Munich kama uwanja wa nyumbani ambazo ni Bayern na 1860 Munich. Uwezo wake ni mashabiki 75,000.

Wembley

Uingereza wanajivunia kwa kiwango kikubwa kuwa na uwanja wa namna hii. Ulifunguliwa mwaka 1923 na kufanyiwa maboresho makubwa mwaka 2007. Uwezo wake sio wa kubezwa ambapo huchukua zaidi ya mashabiki 90,000. Hutumika pia kwa matamasha ya kimuziki mbali na mpira wa miguu.

Estádio Municipal de Aveiro

Taifa linalokuja juu kisoka kwa sasa linamiliki uwanja ambao una heshima kubwa sana duniani. Ureno kwa sasa wana historia kubwa kwenye soka kwa kuwa na wachezaji wenye majina makubwa katika ligi mbalimbali. Uwanja wao huo una uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 30,000.

Bird’s Nest Stadium

Nchi ya China haina historia kubwa sana kisoka lakini wanamiliki viwanja vizuri sana vyenye uwezo mkubwa. Uwanja huu waliujenga 2004 na uwezo wake ni zaidi ya watu 90,000.

3 Komentara

    Ila kweli uwanja wa Africa kusini ni mkubwa,
    Kweli unasifa yakuchezeshwa kombe la dunia,
    Uliweka historia nzuri Africa.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.