Hii ni hatua muhumu kwa kila timu kwenye michuano hii ya Kombe la Mataifa ya Africa -AFCON 2019. Madagascar siyo timu ambayo Tunisia wanatakiwa kuichukulia mchezo mchezo. Naimu Slitti anawaonya Tunisia wakiwa wanaenda kwenye robo fainali ya AFCON 2019.
Tunisia wameshinda AFCON mara moja mwaka 2004, kutokana na mwenendo wa Tunisia kwenye gemu zilizopita Slitti anasema kuwa bado kuna nafasi kubwa ya kufanya mabadiliko hasa kwenye nafasi ya ushambuliaji kati kati kati.
Naimu Slitti ana wasi wasi kwa sababu ya soka analoliita bovu walilocheza dhidi na kuwapumzikia Ghana, ana matumaini kuwa wanaweza kuendeleza moto huo sharti wachukue tahadhari kuelekea pambano dhidi ya Madagascar .
Madagascar wanapewa nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye michuano hii baada ya na kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B na kuwachapa DRC Congo kwenye matuta kwenye hatua ya mtoano wa timu 16.
Wachezaji matata wa kutazamwa zaidi.
Lalaina Nomenjanahary kwa Madagascar
Amechapa jumla ya magoli 7 kwenye mechi 4 za AFCON hapo Misri. Anatarajiwa kuwa ataendelea kufanya maajabu, anapaswa kuchukuliwa kama tishio kwa wataalamu wa Tunisia.
Wahbi Khazri kwa upande Tunisia
Winga huyu wa Saint-Etienne ameshindwa kufanya makubwa sana pale Egypt. Lakini ni mmoja wa wachezaji tishio kwa kikosi cha Tunisia, Madagascar watahitaji kumtazama sana.
Povel tz
Gud news
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa meridianbet