Balotelli Ameondoka Marseille

Nyota Mario Balotelli ameondoka Marseille kufuatia kumalizika kwa kwa mkataba wake klabuni hapo.

Staa huyu lijiunga na klabu ya Marseille akitokea Nice mwezi januri kwa mkataba wa mda mfupi akiwa saidia kumaliza vyema msimu wao. Amewafungia magoli 8 kwenye mechi 15 alizoawachezea Marseille ndani ya Ligue 1.

Klabu hii ilihitaji sana kumbakiza staa huyu lakini kushindwa kwao kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kumewafanya wapunguze bajeti katika malipo ya mishahara.

Raisi wa klabu hii amethibitisha kuondoka kwa Ballotelli huku wachezaji wengine kama Kevin Strootman, Adil Rami naLuiz Gustavo wamekuwa wakihusishwa na uhamisho, huku Lucas Ocampos akiwa tayari ameshaondoa maguu kwenda Sevilla.

Balotelli sasa yupo huru na anatarajiwa kuwa anweza kurejea Italia au Uingereza akihusishwa na klabu za Napoli na West Ham.

Marseille wanatarajia kutafuta mbadala wa kuziba pengo, wanahitaji kufanya kujaza vyema safu ya ushambuliaji na kati kati.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.