Kizazi Kipya cha Barca…

Inaonekana isiwe shida sana kwa kikosi cha Barcelona kuwakosa nyota kama Messi kutokana na uwepo wa wachezaji ambao bado wana nafasi ya kutafuta matokeo uwanjani hata kama wakongwe wa klabu hiyo wanakosekana uwanjani kuipa nguvu timu yao hiyo. Hilo linatokana na matokeo ambayo vikosi hivyo vinapata kwa sasa.

Ansu Fati aliweza kupata goli ndani ya mechi hiyo lakini hakuishia hapo aliendelea kwa kutoa pasi ya goli ambayo iliwapa uongozi klabu yake ya Barcelona kutokana na uwezo wa nyota ambao walikuwepo uwanjani wakiwemo De Jong, Griezmann na wengine wengi ambao ni sehemu ya kikosi hicho.

Ameicheza mechi yake hiyo akiwa na miaka 16 pekee na ameweza kucheza kwa mafanikio makubwa ambayo yamemfanya aweze kuandika historia ya pekee sana uwanjani hapo. Kwa umri wake, ni nyota wachache sana wanaoweza kufanya makubwa kama yake lakini yeye ameudhihirishia ulimwengu kwamba anao uwezo huo.

Ikiwa ni katika wakati ambao Messi hawezi kuingia kusaidia kikosi hicho kupata matokeo lakini halikumpa wakati mgumu kuangalia ndani ya kikosi cha watoto kwa klabu hiyo ili aweze kuwa mbadala wa majeruhi Messi na Dembele, lakini aliweza kuonesha ubora wake ndani ya dakika saba pekee tu baada ya kuwa bora zaidi ya ilivyofikiriwa.

Baada ya kupewa pande nono na De Jong na kuweza kuandika goli la kwanza kwa timu yake hiyo dakika kadhaa baadaye akaamua kurudisha fadhila kwa kumtengenezea De Jong pasi ambayo iliwafanya kuongoza magoli mawili ndani ya mechi hiyo ikiwa ni dakika kadhaa baada ya kufunga goli la kwanza.

Viongozi na makocha ambao wamemfundisha nyota huyo anayechipukia wanasema kwa maisha yao hawajawahi kuona aina ya mchezaji wa umri wake akiwa na kiwango cha pekee kama anachokionesha nyota huyo. Ni aina ya kizazi ambacho kitakuwa na manufaa kwa baadaye ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo henda akawa sehemu ya kizazi kitakachoanza kushuhudiwa ndani ya timu ya taifa ya Hispania ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 17 ambao wataanza kuwa uwanjani mapema mwezi ujao. Inaonekana kabisa kwamba taifa la Hispania wanawania kumyakua nyota huyo.

Nyota huyo ambaye ni raia wa Guinea Bissau alihamia Hispania na familia yake lakini hadi sasa kuna jambo linaendelea kwamba kocha wa Hispania, Moreno anatamani kumchukua nyota huyo awe ndani ya taifa hilo na kuwa kizazi cha Hispania.

Makala iliyopita

2 Komentara

    Habari nzuri sana

    Jibu

    Kweli kabisa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.