Usajili Hatari wa Juventus Kutoka Uingereza

Baada ya fununu za muda mrefu kwamba Ramsey amesaini kuichezea Juventus kwa msimu ujao, mchezaji huyo raia wa Wales amesaini kandarasi inayomweka klabuni hapo hadi 2023; atakuwa analipwa kiwango cha £400,000 kwa wiki na kumfanya mchezaji anayelipwa kiwango kikubwa kutoka taifa lake. Ramsey atakuwa mchezaji wa 15 kusaini klabuni hapo na wazee wa Turin tangu mwaka 2005. Wachezaji wengine waliowika baada ya usajili wao kutoka Uingereza:

Paul Pogba

Ni usajili mzito kuwahi kufanywa na Juventus miaka ya nyuma kidogo. Mchezaji huyo aliipa klabu hiyo kila kinachoitwa ushindani, matokeo na kujituma akiwa uwanjani. Alisajiliwa kutoka Manchester United mwaka 2012 kwa usajili huru. Akiwa amefanikiwa kucheza mechi 178 na kufunga magoli 34 ndani ya mechi hizo katika kipindi chake huko. Na aliweza kurudi tena kujiunga na United 2016 kwa ada ya  £89.3M.

Carlos Tévez

Huu ni usajili mwingine mkubwa kuwahi kufanywa na Juve, wakimsajili kwa ada ya uhamisho ya £12M. Alifanya makubwa sana na klabu yake hiyo na kulipa fadhila za usajili wake ndani ya klabu hiyo. Ambapo alifanikiwa kufunga magoli 50 katika michezo yake 95 aliyoicheza na klabu yake hiyo, lakini pamoja na ushawishi wote baadae aliondoka na kurudi kwao Argentina.

Patrice Evra

Alisajiliwa na Juve baada ya makubaliano na klabu yake ya zamani Manchester United. Aliweza kujiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 33 na kufanikiwa kufanya mengi na klabu hiyo kwa wakati wake wote alipohudumu nayo; kabla ya mkataba wake kuisha na kuweza kujiunga na Marseille baada ya michezo yake 82 na Juve.

Wojciech Szczesny

Huu ni usajili mwingine wa thamani kuweza kufanywa na klabu hiyo kwa wakati wake. Waliweza kumsajili nyota huyo baada ya kutaka kutimka kutoka Arsenal kwa ada ya 12.2M, baada ya kufanya vizuri alipokuwa kwa mkopo na Roma 2017. Kwa sasa ndiye anayetumainiwa ndani ya kikosi hicho chenye nyota wengi sana.

Mohamed Sissoko

Pamoja na kukabiliwa sana na majeraha mchezaji huyo aliweza kufanya makubwa sana na klabu hiyo kwa kuweza kuingia uwanjani katika mechi 100 za klabu hiyo. Aliweza kuwasaidia Juve kubaki imara muda wote kila alipopata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hicho kitu ambacho kimeijengea heshima klabu hiyo hadi hivi leo; kwa kuwa na wachezaji wa aina yake wenye uwezo mkubwa.

3 Komentara

    Usajili mzuri

    Jibu

    Usajili wa maana pia wakiwapata watawasaidia

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.