Kuna wakati timu inaweza ikawa bora lakini kama itakosa wazuiaji wa mipira bora katika milingoti miwili iliyosimama huweza kuwa ni tatizo kubwa zaidi litakaloifanya klabu husika kupoteza uimara wake. Hapa tunakuletea walinda mlango bora zaidi duniani wanaoshika nafasi za kuzuia ndoto za washambuliaji wengi katika ligi kuu ya Uingereza.
David de Gea
Kati ya vitu Manchester United wanjivunia ni kuwa na aina ya golikipa kama huyu. Ni mtu ambaye akiwa golini unajenga imani yako kabisa bila kuwa na wasiwasi wowote. Kwa uhakika anashika nafasi ya mchezaji na golikipa kwa wakati mmoja. Anafanya kazi kubwa ya kufuta madhaifu na makosa mengi yanayofanywa na walinzi wake. Kwa ubora wake ni mtu ambaye hawezi kudhaniwa au kumjadili sana. Katika hilo aliandika historia yame ndefu siku wanakipiga na Spurs kwa kuokoa michomo ya hatari 11 na kuwaacha Dele Alli, Kane na Son midomo wazi kwenye mechi ile. Amekuwa mhimili mkubwa sana katika klabu hiyo.
Lukasz Fabianski
Ukitaka kuzungumzia suala la ubora huwezi kusahau kuzungumzia ubora wa mchezaji huyu wa West Ham amekuwa akiisaidia sana klabu take kupata matokeo mazuri, kwa kuzuia mipira mingi isipite kwake. Pamoja na uinara wa Wes ham hapa karibuni lakini amekuwa nguzo kuu kuifanya klabu hiyo imara zaidi hadi sasa kwa kufanya makubwa zaidi. Hakika ni zao ambalo klabu hiyo inapaswa kulitunza maana kuondoka kwakw kutawapoteza sana.
Alisson Becker
Huu ni usajili wa maana sana Liverpool wameufanya, hadi sasa ameachia mipira 11 tu kutikisa nyavu zake kwenye ligi. Sio kitu cha mchezo kufanya hivyo kwa sababu ikiangaliwa kwa namna ligi inavyokwenda na ilivyoanza imekuwa na upinzani sana ambao hakika unawafanya wengi kupoteza ubora wao, lakini kwake pamoja na kuwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi hiyo kwa sasa anafanya makubwa yanayoonesha ukomavu mkubwa alio nao. Amechangia makubwa hadi kwa nafasi aliyo Liverpool kwa sasa.
Ederson
Wengi wanasema golikipa amekuwa akibebwa na safu yake ya ulinzi kutokana na kuwa imara sana, lakini kiuhalisia yeye kama sehemu ya mchezo ndiye anayetengeneza safu nzima ua ulinzi. Amefanya makubwa sana na klabu hoyo hadi kuipa ubingwa msimu uliopita hadi sasa klabu hiyo bado ipo katika nafasi ya kushindania ubingwa. Ameweza kuzuia kufungwa kabisa [clean sheets] katika mechi tisa ndani ya msimu huu. Hii ni heshima kubwa kwake ikikinganishwa na ugumu wa ligi yetu kwa sasa ulivyo. Kutokana hilo kunamfanya asalie kuwa bora.


Issa
Walinda