Kila kocha anapokuwa katika klabu fulani kufundisha huwa na nia kubwa moja ya kutaka kufanya vizuri na kuweza kufahamika zaidi kwa matunda na kazi kubwa anayoifanya. Zaidi ya hayo huwa na nia ya kuweza kuonesha uwezo wake wa kufundisha soka na kila mmoja akaheshimu nafasi yake kiushindani.
Japo hutokea wakati ambapo kocha huyo anashindwa kufikia malengo ambayo klabu yake inakuwa ineyaweka au hata yeye mwenyewe anakuwa ameyaweka kwa kipindi chake akiwa kama mwalimu wa timu hiyo. Jambo kama hilo huweza kuwa gumu kuweza aidha kuvumilika kwa wamiliki au hata yeye mwenyewe kujishauri juu ya matokeo yake.
Baada ya hali hizo hupelekea kuweza kujishusha kabisa kiuwezo au watu wa pembeni ambao wanaangalia kile kinachofanywa kudharau nafasi hiyo kwa kuona kwamba sio nafasi yake kuweza kufanya vizuri kwenye nafasi hiyo. Jambo kama hilo humfanya kocha huyo aweze kuchukuliwa kawaida sana kiutendaji.
Mbali na hapo wafuatao ni baadhi ya makocha ambao wamekosa kabisa kuuza Ulaya pamoja na kufundisha soka lenye mvuto lakini nafasi yao kwa sasa inaonekana kama haipo kutokana na utawala wa warithi wao kuweza kufanya makubwa zaidi yaliyofunikwa na kile walichokifanya wao kwa kipindi chao chote.
Bruce Rioch, ili kuweza kutambua nafasi yake ni lazima mmoja aweze kujiuliza swali hili: Klabu ya Arsenal iliongizwa na nani kabla ya Wenger? Jibu la swalj hili litatupeleka moja kwa moja kutambua nafasi aliyokuwa nayo kocha huyo katika kipindi kukiwa na watu kama Ian Wright ndani ya ardhi hiyo ya Emirates. Lakini kwa sasa ni vigumu sana kukumbuka nafasi yake kutokana na kuwepo kwa Wenger ambaye ameweza kufuta kabisa uwepo wa mtangulizi huyo. Jambo hilo kwa hakika limeweza kumpoteza kabisa mwalimu huyo na kuondoa uwepo wake kwa kizazi cha soka cha sasa.
Alan Ball, mkongwe aliyeweza kuzitumikia klabu za Southampton na Manchester City kwa kipindi chake cha kufundisha soka. Anakumbukwa kwa mfumo wake ambao alipenda kuutumia mara zote wa 4-4-2 ambapo ulionekana kuwa na matunda lakini kwa falsafa yake ulikuwa ni mgumu sana kupata matokeo. Miongoni mwa kitu hakiwezi kusahaulika kwake ni kwamba alikuwa ni mvhezaji zaidi ya kocha kwa sababu akiwa kama mchezaji alifanya makubwa zaidi ya alipokuwa kocha.
Brendan Rodgers, aliweza kuhudumu katika klabu kubwa nchini Uingereza na kuwa na matokeo mazuri sana lakini kwa sasa waliweza kusahaulika kabisa kuwa kama ni mtu ambaye anahistoria kubwa. Hata kipindi cha uongozi wake hakuweza kupata heshima ike inayostahili sana kwa nafasi yake. Aliweza kufanya kazi akiwa kama kocha wa Swansea City na Liverpool na katika kipindi chake chote aliweza kufanya mazuri yanayofaa kusifiwa sana.

