Shkodran Mustafi anaamini amenufaika na kucheza mechi nyingi tangu Mikel Arteta alipotua Arsenal msimu huu, japo mustakabali wake haujafahamika.
Mustafi 27 aliambiwa huenda angeondoka dirisha la majira ya joto lililopita na kocha aliyepita Unai Emery na jina lake halikuwepo kwenye mchezo Ligi Kuu wowote tangu mwishoni wa Novemba.

Mkataba wa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani unamalizika June 2021.
“Nimecheza mara nyingi chini ya Mikel Arteta, pia katika Ligi kuu. Hii imenisaidia sana. Najisikia vizuri sana sasa. Naelewa aina yake ya mpira, jinsi anavyotamani tucheze, inanifiti mimi,”
“Ni kiongozi mzuri, najihisi hivyo kwa kipindi kifupi nimejifunza vitu vipya vingi vilivyo nisaidia kwenye uchezaji wangu.

“Naona nikiendelea kucheza katika kikosi chake. Lakini bado sijajua mustakabali wangu, bado kuna viulizo vingi.”
Mustafi amekuwa mchezaji muhimu Arsenal tangu Arteta alipojiunga na klabu yake ya zamani kama Kocha mkuu.
Pamoja na kuonekana ameimarika akiwa na jezi ya Arsenal, Mustafi bado ana mashaka na mustakabali wake hasa baada ya mlipuko wa virusi vya Corona kwenye nchi za Ulaya.
“Kila mtu ana wasiwasi juu ya hali ya sasa na sio kufikiria maswala binafsi ya wakati ujao,” ameongezea.
“Jambo la msingi natamani nicheze mpira tena. Ndio wote tunavyojisikia, tunatamani kurejea uwanjani. Kuna maswali mengi kwa sasa.


Furahav
Pambana sasa,upate namba.
Ester jackson
Hivi kwanini hakukamilishiwa na imeishiaje