Wanamichezo wengi wakubwa wanapostaafu kwenye mchezo fulani huwa na ndoto ambazo hutamani kuziishi katika maisha yao ya baadae. Wengine huendeleza michezo yao waliyokuwa wanaicheza kwa namna fulani: na wengine huamua kuachana kabisa kujihusisha na michezo. Wenye nia ya kuendeleza michezo hiyo huweka jitihada fulani ili kuandaa mazingira ya wao wanataka kuwa na athari gani chanya kwa wengine wanaopenda michezo hiyo.
Mieleka ikiwa sehemu ya michezo inayoangaliwa sana, inemtendea Shawn kile alichokuwa akikitamani siku nyingi kukifikia, sio hivyo tu pia anaona njia hiyo inamsaidia yeye kuwapa vijana wengine kile kilichomfanya yeye kufikia hapo, ikiwa pia ni ndoto yake kufanya kitu kitajachowasaidia wengine kufanya kitu cha ndoto zao.
Tangu astaafu kwenye mieleka amekuwa akifundisha wenye nia ya dhati katika mchezo wa mieleka kwenye kituo cha Orlando ambacho kinaidadi kubwa ya vijana wenye ndoto za kucheza mieleka.
Michael anaona kwake yeye kufanya chenye athari chanya kubwa kwa kizazi kijacho ni kitu kikubwa na imani hiyo inamjenga yeye kika siku. Na hana kitu cha pekee kinachomsukuma yeye kulifanya hilo bali ni mapenzi tu ya dhati aliyonayo kwenye mchezo huo, na nia yake ya kufijisha wengi kwenye mafanikio; hivyo ni kitu anachokifanya kwa moyo wote.
Mwana mieleka huyu ana umri wa miaka 53, amakuwa katika mchezo huo kwa miaka 34. Amepata mafanikio makubwa sana akiwa ameshinda mkanda wa dunia mara nne [4], mafanikio mengine ni kuwa katika jumba la watu wenye historia na mafanikio makubwa kwenye mieleka wanaofahamika kama WWE Hall of Famer akibatizwa jina la Mr. WrestleMania: katika jumba hilo yupo na wanamichezo wenzake wengine kama Bret Hart anaefahamika kama ‘Stone Cold’, Steve Austin, The Undertaker, Razor Ramon, Ric Flairi na wengineo.
Hawa ni tunu kubwa katika mchezo huu.
Shawn bado hajaridhika tu pamoja na mafanikio hayo, anatamani umri wake ungekuwa rafiki ili akamilishe kabisa vile baadhi alivyoshindwa kuvifanya. Pamoja na hayo anaamini kupitia vijana alionao atawafanya waweze kuvifanya vitu hivyo. Anaamini sio wakati wake kurudi ulingoni na kuweza kupigana, ni wakati wa kuwaachia vijana nao waweze kuona namna gani watafanikiwa kuziishi ndoto zao.
Anaongeza kwa kusema kwa sasa yeye na wenzake wanachofanya ni kukaa mezani kwa pamoja, kupandikiza mbinu na mawazo yao, kuandaa mapambano na kuangalia kitu chenye upekee kitakachowafanya wao bora zaidi ya wengine.


Zeiyana
Anafanya vizuri Shawn haonesha kabic kama hataki michezo ya mireka hipotee dunia safi sana