Willian amesema anahitaji kubaki Ligi kuu ya Uingereza kama mkataba wake na Chelsea ukiisha majira ya joto.
Mbrazili huyo ameshindwa kufikia makubaliano na Chelsea, na ameongeza kuwa majadiliano “yamesimama”.
Arsenal na Tottenham wameonyesha nia ya kuhutaji huduma ya winga huyo wa Brazil.

“Natamani kubaki Ligi Kuu ya Uingereza, lakini sio nakataa kucheza ligi zingine,” amesema Willian. Nitacheza mpaka mwisho wa msimu alafu tutaangalia nini kitatokea. Nimezoea maisha ya Uingereza. Sifikirii kurudi Corinthians kwasasa. Lengo langu ni kubaki Ulaya.”
Willian ameongeza: “Nahisi nipo kwenye ubora wangu wakati huu. Wachezaji wakuwa vizuri wakicheza na nadhani niko vizuri sasa.”
Akijiunga na Tottenham tutaona Willian akiwa pamoja na kocha wake wa zamani Jose Mourinho.
“Tuko vizuri na Mourinho, nimejifunza nikiwa chini yake na tumebaki marafiki,” amesema Willian. Bado tunawasiliana sana, lakini hatujaonana hivi karibuni. Sijamuona tangu arejee London.”


Furahav
Baki tu hapo.
Povel
Gud news