Wakati wapenzi na wafuatiliaji wa soka duniani kote wakitolea macho tetesi za Jack Grealish kukimbilia kunako klabu ya Mnachester United zimeibuka habari za mchezaji huyo kukiuka Agizo la Selikari la kuepuka mikusanyiko isiyo na ulazima. Nyota huyo ambae pia ndio Nahodha wa timu ya Aston Vila ambayo kwa sasa mtanzania Mbwana Ally Samatta anaitumikia, Grealish alikiuka agizo hilo kwa kutoka na gari yake aina ya Range Rover, ambapo imeripotiwa kupata ajali ya kuharibu magali mawili yaliyoko pembezoni mwa barabara katika jiji la Birmingham.
Masaa machache kabla ya tukio hilo Grealish alimpost kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kumtakia heri aliyekua mchezaji wa zamani wa Aston Villa Ross McCormack. Kabla ya post hiyo Grealish alipost kupinga watu wanao hamasisha utaratibu wa kubaki nyumbani ili kujikinga na janga la Corona.

Wakati timu yake ya Aston Villa kuonesha kuchukizwa na tukio hilo na kutoa tamko la kuto kufurahishwa kabisa na nyota huyo, timu ya Manchester United kwa kupitia kocha wake Ole Gunnar Solskjaer imeibuka kwa kusema mpango wao wa kumnyakua Kiungo huyo kwa kuongeza dau mpaka kufikia Pauni milioni 80 na kuongezea kua mpango huo utakamilika ndani ya wiki chache zijazo.


Gabriel
Habar njema sana 👍