John McDermott: Nitampga Tyson Furry

John McDermott atabaki kwenye vitabu vya historia baada ya kumtwanga Tyson Furry kwa point kwenye pambano lao lililo fanyika mwaka 2009, lakini hayo yalisha pita na kwasasa Tyson Furry ndie mfalme wa masumbwi kwa sasa.

“Ni kweli inaniumiza, na sina maana kwamba labda ningekua bingwa wa dunia lakini huenda ingefanya maisha yangu kua mazuri, ningekua na pesa za kutosha kwa maana kwa kipindi kile hakukua na pesa nyingi kwenye Boxing ukilinganisha na sasa ambapo Furry ni Millionaire na mimi bado nahangaika”. Alisema McDermott ambae kwa sasa ni mfanyakazi wa shirika la reli nchini Uingereza.

John McDermott (kushoto) akiwa na Tyson Fury.

Furry akiwa na miaka 21 tu huku akiwa na kiu ya kuchukua ubingwa wa Masumbwi kwa uzito wa juu kwake ndo lilikua pambano lake la kudhihirishia ulimwengu kua yeye ndie mfalme wa mchezo wa masumbwi ajae.

Huku McDermott akiwa naumri wa miaka 30 akiwa tayari amepambana maopambano kadhaa huku mawili yaliyopita akiwa amepoteza. Ubingwa wa uzito wa juu kwa Furry ndio ulikua wamuhimu kwa kipindi hicho na ilikua ndio kipimo sahihi kwa Furry kukutana na bondia mkubwa na mzoefu kwa kipindi hicho kama John McDermott.

Acha ujumbe