UEFA wanatarajia kufanya maamuzi juu ya kumaliza Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa. Kutokana na hali halisi ya sasa, nchi nyingi Ulaya ziko kwenye zuio la kutokuondoka nyumbani na pia mipaka imefungwa kwa baadhi ya nchi kupunguza hatari ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Hata hivyo, UEFA wanafanya mkutano kwa njia ya video ili kufanya maamuzi juu ya hatma ya Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa. Awali ilitarajiwamichuano hii ingefika tamati mwezi Juni, tarehe 30, lakini bado kumeendelea kuwa na sintofahamu na wasiwasi zaidi. Uongozi wa shirikisho hili barani Ulaya, unaohusisha wanachama wake 55 wanajaribu kufanya maamuzi leo kusogeza fainali zifanyike mwezi Agosti.

Wakati wakifikiria namna bora ya kumaliza michuano hii huku kukiwa na athari kubwa ya virusi vya Corona duniani kwote, UEFA hawafikirii kutomaliza michuano hii mwaka huu. Michuano yote miwili ipo kwenye hatua za mtoano kwa timu 16, na kwao ni lazima michuano iishe.
Mabadiliko yatakayotokana na maamuzi ya leo yanakwenda kuathiri kabisa msimu ujao, kitu ambacho hakiepukiki kwa sasa. Isipokuwa ni mpango thabiti wa kuweka ratiba na namna ya kukabiliana na mabadiliko kadri yatakavyotokea.


David pere
Ni muhimu kutoa maamuzi yaliyo sahihi na yenye faida kwa timu zote
Issa
Safi sana