FIFA wameahidi kuwa watatoa pesa kiasi cha Euro bilioni 2.6 kwa ajili ya kuokoa soka kutokana na janga la virusi vya Korona.
Kutokana na Janga la virusi hali imekuwa ngumu sana miungoni mwa karibia klabu zote ulimwenguni baada ya michezo kusimama, huku mikusanyiko ikiwa imezuiliwa kabisa kwa nchi nyingi.
Klabu nyingi zimekuwa zikijiendesha kupitia mapato ya viwanjani na shughuli zingine aq biashara walizowekeza. Kwa bahati mbaya Janga la virusi vya Corona limeathiri karibu shughuli zote za kicuchumi na kijamii hivyo kuacha vilabu vikiwa na mapato kidogo sana kuweza kumudu uendeshaji na malipo ya wachezaji.
Kufuatia changamoto hii, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limeweka wazi kuwa wanatarajia kutoa Euro bilioni 2.6 ili kunusuru hali ya soka ulimwenguni. FIFA wanasema shirikisho hili ni shirikisho linalojiweza kifedha na ndiyo tegemeo la wadau wa soka pindi wanapokuwa na shida. Wakati huu wa ukata kwa vilabu vingi, FIFA itawashika mkono wale waliokuwa na uhitaji zaidi.
Kutokana na hali kutokuwa shwari zaidi, baadhi ya vilabu vimeamua kuwapunguzia malipo wachezaji na watumshi wao wasio wachezaji kwa asilimia fulani, huku wachezaji wakiridhia ili kunusuru uendeshaji wa timu hizo.
Hofu iliyopo kwa Vilabu.
Kwa asilimia kubwa wadhamini wa Vilabu ni wafanya biashara, na kwa hali iliyopo wengi wao biashara zimeyumba kupita kiasi, hivyo watakuwa wanafikiria zaidi namna ya kunusuru biashara zao kuliko vilabu. Pia wapenzi wa vilabu hivi bado watakuwa wanafikiria hatma yao kupambana na changamoto zilizokuja na zitakazobakia baada ya kukabiliana na janga hili hivyo kuna wasi wasi pia hali ya kiuchumi ya wapenzi wa Vilabu haitawaruhusu kutoa mchango wao kama awali.
Ni wakati muafaka kwa FIFA kuwashika mikono wanasoka, soka litaendelea kudumu!
“Sisi ni taasisi yenye nguvu kifedha, ni jukumu letu kutoa msaada unaohitajika kwo katika wakati huu wa uhitaji. Jumuiya ya soka inakumbana, kwa kadri au kiasi kikbwa na tatizo la fedha kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona.”


Issa
Vizuri sana fifa mnatoa hamasa kwa vyama vingine katika kuinua soka
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa meridianbet
farida ahmadi
Asante kwa taarifa meridianbettz